Home Mchanganyiko HABARI KATIKA PICHA : UJUMBE WA TANZANIA NCHINI CAPE VERDE KATIKA KUTANO...

HABARI KATIKA PICHA : UJUMBE WA TANZANIA NCHINI CAPE VERDE KATIKA KUTANO WA KIMATAIFA WA UTALII

0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimuonesha  baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo katika jarida la Utalii kutoka Tanzania Waziri wa Utalii wa Hispania, Maria Illerakabla ya kumkabidhi zawadi ya majarida yanayoelezea utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano wa  64  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika  kwa muda wa siku nne  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  akimkabidhi zawadi ya Kijitabu cha misitu kinachoelezea fursa za uwekezaji katika maeneo  ya misitu nchini Mhe. Ngobitizitha  Ndlovu (kushoto)  mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika  kwa muda wa siku nne  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( katikati ) akiwa kwenye picha ya pamoja  na Waziri wa Utalii na Mambo Kale Zanzibar, Mhe.Lela Mussa Mohamed (kushoto)  pamoja na Waziri wa Utalii wa Morroco Mhe.Nadia Fettah  ( kulia)   mara baada  kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa  Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika  kwa muda wa siku nne  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiagana na Waziri wa Utali Cape Verde, Mhe. Carlos Santos  akiagana na Waziri wa  Utalii wa Cape Verde….. ambapo wamekubaliana katika kubadilishana uzoefu katika kukuza utalii