Home Michezo SIMBA SC YATAMBULISHA JEZI ZAO MPYA ZA MSIMU 2021-2022

SIMBA SC YATAMBULISHA JEZI ZAO MPYA ZA MSIMU 2021-2022

0

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Simba Sc imetaambulisha jezi zao mpya kwaajili ya msimu ujao ambapo katiika jezi hizo kuna jezi ya nyumbani ambayo ni nyekundu pamoja na jezi za ugenini ambazo ni nyeupe na nyeusi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ezekiel Kamwaga. amesema mapokezi ya jezi hizo yanatarajiwa kuwa makubwa kulingana na maombi ya jezi hizo.

“Maombi ya jezi kutoka kwa mashabiki wa Simba yamekuwa makubwa sana na uongozi umeona ni vyema kuwasikiliza. Natangaza rasmi kwamba kuanzia sasa jezi mpya za Simba zinapatikana sasa kwenye maduka ya Vunja Bei nchi nzima.”- Ezekiel Kamwaga. #SimbaDay2021 #NguvuMoja