Home Biashara KAMPUNI YA WORLD LOGISTICS COMPANY LIMITED YATAMBULISHA HUDUMA YA CARGO PICKUP AND...

KAMPUNI YA WORLD LOGISTICS COMPANY LIMITED YATAMBULISHA HUDUMA YA CARGO PICKUP AND DERIVERY SERVICES KUMLINDAA MTEJA WAO DHIDI YA UVIKO 19

0

Afisa Masoko wa Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC) Bi.Apaisaria Godvice akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitambulisha huduma yao mpya inayoitwa Cargo Pickup and Derivery Service ambayo itawasaidia wateja wao kuagiza na kuletewa mzigo moja kwa moja pale alipo kutoka nchi yoyote Duniani.

Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC) Bi.Agnes Daniel akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitambulisha huduma yao mpya inayoitwa Cargo Pickup and Derivery Service ambayo itawasaidia wateja wao kuagiza na kuletewa mzigo moja kwa moja pale alipo kutoka nchi yoyote Duniani.

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kutokana na janga la Uviko 19 linalosumbua Duniani,Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC) ambayo inajishughulisha na usafirishaji wa mizigo ya aina zote ndani na nje ya nchi wametambulisha huduma ya Cargo Pickup and Derivery Service ambayo itawasaidia wateja wao kuagiza na kuletewa mzigo moja kwa moja pale alipo kutoka nchi yoyote Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Masoko wa kampuni hiyo Bi.Apaisaria Godvice amesema huduma hiyo itasaidia kuepuka usumbufu, gharama za safari, hoteli na michakato mingine ambayo itamgharimu fedha na muda.

“Huduma hii ni muhimu kwa wateja wetu kwani itamsaidia pia kuwa salama dhidi ya maambukizi ya gonjwa hili hatari linalosambaa kwa kasi na kuua ndugu zetu”. amesema Bi.Apaisaria

Amesema kupitia teknolojia, muagizaji ataweza kufuatilia mzigo wake katika hatua zote za usafirishaji tangu siku anayoagiza hadi siku anaupokea kwa nyenzo ya Google Exces Spreadsheet.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC) Bi.Agnes Daniel amesema mteja anatakiwa kuwasiliana na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ambapo atakutana na namba ambayo akipiga moja kwa moja anaweza kusikilizwa na kupata huduma stahiki.