Home Michezo KOFFI OLOMIDE AWASILI KUWATUMBUIZA WIKI YA MWANANCHI KESHO UWANJA WA MKAPA DAR

KOFFI OLOMIDE AWASILI KUWATUMBUIZA WIKI YA MWANANCHI KESHO UWANJA WA MKAPA DAR

0

MWANAMUZIKI nguli barani Afrika, Koffi Olomide amewasili leo Dar es Salaam kutoka kwao, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tayari kutumbuiza kwenye tamasha la klabu ya Yanga lijulikanalo kama kilele cha Wiki ya Mwananchi kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini.
Pamoja na Koffi, kwenye tamasha hilo pia watakuwepo wasanii wengine mbalimbali wa nyumbani, akiwemo Nandy, Wanaume Family TMK na Chegge.

Tamasha hilo ni maalum kwa Yanga kuzindua rasmi msimu mpya kwa kutangaza kikosi chake pamoja na jezi itakazotumia nyumbani na ugenini msimu ujao.
Kutakuwa na mechi za vikosi vya Yanga kuanzia vya vijana, wanawake na maveterani kabla ya utambulisho wa kikosi cha msimu mpya kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco ya Zambia Saa 1:00 usiku.