Home Mchanganyiko MHE.MAKINDA ATOA ELIMU YA SENSA KWA WAKAZI MAKETE

MHE.MAKINDA ATOA ELIMU YA SENSA KWA WAKAZI MAKETE

0
************************
NJOMBE

Wakati ofisi ya takwimu ya taifa(NBS)ikiteua mikoa 13 ukiwemo Njombe kufanya sensa ya majaribio kwa ajili ya maandalizi ya sensa inayotarajiwa kufanyika 2022 ,Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Tanzania bara Anna Semamba Makinda ametoa rai kwa watanzania kuepusha siasa katika zoezi hilo kwa maslahi ya taifa.

Rai hiyo ameitoa wilayani Makete mkoani Njombe alipokutana na wananchi pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuwaeleza umuhimu wa zoezi hilo ambalo katika mkoa wa Njom e serikali imeteua kitongoji cha Dombwele .

Makinda amesema kupitia takwimu za sensa ya watu na makazi serikali inapata takwimu halisi za watu wake na kuweka mipango madhibuti ya maendeleo.

“Nipende kutoa rai kwa wananchi kuondoa siasa katika utekelezaji wa zoezi hili la majaribio ya sensa na makazi kwa kuwa linamanufaa makubwa kwa nchi,Alisema Anna Makinda.

Awali Said Amiry ambaye ni afisa habari kutoka ofisi ya takwimu taifa amesema sensa ya sasa imeboreshwa zaidi ambapo kaya zitakuwa zikiulizwa takribani maswali 90 ili kupata taarifa zote muhimu ambazo zitasaidia serikali kufanya mipango yake ipasavyo.

Aidha afisa huyo amesem eneo lingine ambalo limeboreshwa ni ukusanyaji wa taarifa katika ngazi ya kitongoji ambapo kwasasa kitongoji kimefanywa kama eneo mojawapo la kuhesabu watu tofauti na mara ya kwanza ambapo kitongoji kilikuwa kikigawanywa sehemu mbalimbali.

Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Dombwela waliofika kupatiwa elimu hiyo akiwemo John Sanga  wameipongeza serikali kwakuchagua kitongoji cha Ndombwele kufanyia jaribio la zoezi hilo na kuhitaji kueleweshwa kuhusu wasafiri siku ya sensa na watu wenye makazi yasio ya kudumu.

“Tunashukuru kwa mpango huu kwakuwa utaleta manufaa kwa serikali na wananchi lakini tunaomba tuelimishwe kuhusu umuhimu wake na namna wasafiri watakavyohesabiwa siku hiyo,Alisema John Sanga .

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akasema kwa kuwa mpango huo umebeba mipango ya serikali ,unakwenda kusimamiwa ipasavyo kwa ushirikiano wa karibu na wakuu wa wilaya ya wakurugenzi ili serikali iwe na uwezo wa kutekeleza mipango ya maendeleo ya muda mrefu na mfupi bila changamoto yeyote.

“Mimi nitashirikiana na wakuu wote wa wilaya na wakurugenzi ili kufanikisha zoezi hilo la sensa ya majaribio wilayani Makete.’Alisema Rubirya .