Home Mchanganyiko MKURABITA YATOA MAFUNZO KWA  WAKULIMA ILI WAWEZE KUTUMIA ARDHI ILIYORASIMISHI KUFANYA KILIMO BIASHARA

MKURABITA YATOA MAFUNZO KWA  WAKULIMA ILI WAWEZE KUTUMIA ARDHI ILIYORASIMISHI KUFANYA KILIMO BIASHARA

0

Meneja Urasilimishaji Ardhi ma Rasilimali  vijijini kutoka  Ofisi ya Rais ,Mpango wa Kurasimisha Rasimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Anthony Temu akitoa leo elimu kwa wakazi wa Kijiji wa Ukondamoyo wilayani Sikonge juu ya matumizi ardhi iliyorasimishwa kupata mikopo katika Taasisi za Fedha ya kufanya kilimo biashara.

Diwani wa Kata ya Kipanga,Yuda William,akieleza leo jinsi mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima waliorasimishiwa ardhi zao yaliyotolewa na Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania kuimarisha kilimo biashara.

 Picha na Tiganya Vincent

****************************

 

NA TIGANYA VINCENT

 

MPANGO wa Kurasalimisha Rasimali na Biashara za Wanyonge nchini (MKURABITA) umeshauri wakulima  kutumia fursa ya ardhi iliyorasimishwa kujenga mitaji ya kupata mikopo ya kuendesha kilimo biashara ambacho kitawainua kiuchhumi.

 

Kauli hiyo imetolewa leo katika Kijiji cha Ukondamoyo ,wilayani Sikonge na Meneja Urasilimishaji Ardhi ma Rasilimali  vijijini kutoka  Ofisi ya Rais ,MKURABITA Anthony Temu wakati wa utoaji wa elimu ya kuwajengea uwezo Wakulima waliorasimisha ardhi zao.

 

Alisema baada ya kuwajengea uwezo wanalenga kuwaunganisha  wakulima waliorasimishiwa ardhi zao na Taasisi za fedha ili waweze kutumia hati hizo za kimila kupata mikopo ambayo itawasaidia kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo biashara.

 

“Ndugu zangu msiogope kutumia fursa zinazowafikia kama hii ambapo tayari mnazo hati za kimila ili kukopa kwa ajili ya kubadilisha maisha yenu na kujiletea maendeleo”alisema

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge,Hussein Mchomvu, aliwataka wakulima kuongeza thamani ya mazao yao mashambani kwa kulima mazao ya kimkakati kama korosho ambalo ni zao la kudumu.

Diwani wa Kata ya Kipanga,Yuda William,alisema tangu zamani wakulima hawajanufaika na ardhi yao na kuwa mafunzo yanayotolewa na Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania  utabadilisha maisha yao.

Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, MKURABITA wapo mkoani Tabora kutoa mafunzo kwa wananchi vijijini kuhusu mpango huo unavyoweza kubadilisha maisha yao baada ya kurasimisha ardhi yao na kuiongezea thamani.