Home Mchanganyiko RC MKIRIKITI: SERIKALI ITAKAMILISHA MIRADI YOTE KIPORO RUKWA

RC MKIRIKITI: SERIKALI ITAKAMILISHA MIRADI YOTE KIPORO RUKWA

0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti (aliyevaa suti ya blu) akiongea na walimu wa shule ya sekondari Kirando leo alipofanya ziara wilaya ya Nkasi kuhamasisha kazi za maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti akizungumza na wananchi wa kijiji Kirando wilaya ya Nkasi leo ambapo amewahakikishia kuwa serikali itakamilisha ujenzi wa daraja lililobomolewa na maji hivyo kutenganisha kijiji hicho na kijiji cha Kizombe kunakosababisha usumbufu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti  (kushoto) akizungumza na watumishi wa halmashaurinya wilaya ya Nkasi leo alipokagua mradi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nkasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joseph Joseph Mkirikiti akiwa kwenye ukaguzi wa miundombinu ya shule ya sekondari Milundikwa wilaya ya Nkasi ambapo ameagiza viongozi kuhamasisha upandaji miti ili kutunza mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joseph Joseph Mkirikiti  akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi  Peter Lijuakali (kulia) leo alipokuwa akizungumza na walimu wa shule ya msingi Ntanganyika iliyopo Namanyere ambapo ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuboresha miundombuni ikiwemo madarasa ili wanafunzi wasome kwenye mazingira mazuri.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

…………………………………………………………………

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti leo (19.08.2020) amefanya ziara ya kuhamasisha wananchi kuendelea kufanya kazi kwa jitihada huku serikali ikiahidi kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi .

Ziara hiyo imemfikisha Mkuuhuyo wa Mkoa kwenye wilaya ya Nkasi ambapo amekagua miradi ya barabara, maji, elimu na afya iliyoibuliwa na kuanzishwa na wananchi .
“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha miradi yote kiporo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi inakamilika ndio maana imeendelea kutoa fedha za maendeleo” alisema Mkirikiti  alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Kirando.
Kuhusu suala la elimu, Mkuu huyo wa Mkoa amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka waongeze jitihada, ubunifu na uzalendo ili kiwango cha elimu kipande zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijuakali amesema wameweka mpango wa kuhakikisha miradi ya wananchi inakamilika ikiwa bora kwa kuzingatia maelekezo ya serikali
Lijuakali amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia kwa karibu kazi za wananchi ikiwemo miradi ya kipaumbele ikiwemo elimu na afya ili kero za wananchi zipate suluhu.
“Nimejipanga kwa ushirikiano na wakuu wa idara wa halmashauri kukamilisha kwa ubora miradi ya maendeleo huku tukihakikisha maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali tukiyatekeleza kwa haraka” alisisitiza Lijuakali.