Home Mchanganyiko PWANI YAKATALIWA MRADI MMOJA KATI YA 87 ILIYOPITIWA NA MWENGE MAALUM

PWANI YAKATALIWA MRADI MMOJA KATI YA 87 ILIYOPITIWA NA MWENGE MAALUM

0
**************************
Agost 18
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
Mwenge Maalum wa Uhuru mwaka huu umekataa kufungua mradi mmoja kati ya miradi 87 yenye thamani ya bilioni 57.3 ,iliyotembelewa mkoani Pwani,ukiwa ni mradi wa ujenzi wa maabara ya biolojia katika shule ya sekondari ya DUNDA  wilayani  Bagamoyo .
Mradi huo umekataliwa agost 11, baada ya kukosekana kwa taarifa ya mkandarasi inayoonyesha  thamani halisi iliyotumika kujenga maabara hiyo.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru, luteni Josephine Mwambashi amefikia maamuzi ya kutofungua maabara hiyo baada  kukagua mradi huo na kubaini kuna mkanganyiko mkubwa  wa taarifa  za matumizi ya fedha  halisi  zilizotumika wakati wa ujenzi ,pamoja na  maabara  nyingine  17 zilizokuwa zinajengwa  na halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kabla haijagawanywa na kuwa na halmashauri ya Bagamoyo na Chalinze.
Aliiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU  kuchunguza mradi huo  na taarifa za awali ziwasilishwe kwake kabla ya tarehe kumi na nane mwezi huu.
Hata hivyo Mwambashi ametaka wanafunzi waruhusiwe kutumia maabara hiyo wakati uchunguzi ukiendelea.
Awali mwalimu mkuu wa shule hiyo ADEODATA NKWERA amesema mradi wa ujenzi wa maabara  ya biolojia  katika shule ya skondari Dunda  umegharimiu sh. milioni 55 .
Mwenge huo ,umemaliza mbio za zake katika wilaya ya Mafia mkoani Pwani ambapo agost 18 ,mkuu wa wilaya ya Mafia Mhandisi Martin Ntemo alimkabidhi mkuu wa mkoa wa Pwani na kisha kuukabidhi Dar es salaam katika wilaya ya Ilala.