Home Siasa HICHILEMA ASHINDA KITI CHA URAIS NCHINI ZAMBIA

HICHILEMA ASHINDA KITI CHA URAIS NCHINI ZAMBIA

0

************************

Kiongozi wa Upinzani nchi Zambia kupitia chama Cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema ameshinda kiti cha Urais kwenye Uchaguzi Mkuu nchi humo.

Hichilema ameibuka mshindi baada ya kujizolea kura 2,810,777 akimbwaga mpinzani wake kutoka chama tawala Edgar Lungu aliyepata kura 1,814,201.

Hivi karibu kabla ya Tume ya Uchaguzi nchini Zambia Lungu alidai kwmaba Uchaguzi huo haukuwa huru na haki.

Lungu alisema kwamba maafisa wa Chama chake Cha Patriotic Front walifukuzwa kutoka katika vituo vya kupigia kura, wakiacha vituo hivyo pasipokuwa na ulinzi wa kura.