Home Mchanganyiko MAJALIWA AKAGUA KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA MVOMERO NA KITUO CHA KUPOOZEA UMEME...

MAJALIWA AKAGUA KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA MVOMERO NA KITUO CHA KUPOOZEA UMEME CHA MSAMVU MOROGORO

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Meneja Mkuu wa kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills, Eric Cormack kilichopo, katika Wilaya Mvomero, Mkoani Morogoro, wakati alipotembelea kiwanda hicho,

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills, kilichopo, katika Wilaya Mvomero, Mkoani Morogoro, wakati alipotembelea kiwanda hicho

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati Medard Kalemani (kushoto), wakati alipokagua kituo cha kupoozea umeme, kilichoungua moto cha Msamvu ,Morogoro

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mitambo iliyoathirika na moto, wakati alipokagua kituo cha kupoozea umeme, kilichoungua moto cha Msamvu ,Morogoro, Agosti 14, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

………………………………………………………

MAJALIWA AWATAKA WATENDAJI TANESCO WAZINGATIE WELEDI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wataalam wanaosimamia vituo vya kupoza umeme nchini kuwa makini na kuzingatia weledi katika usimamiaji wa vituo hivyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwa wananchi na hasara kwa Serikali .

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (jumamosi, Agosti 14, 2021)  alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha Msamvu Mkoani Morogoro ambacho kilipata hitilafu Agosti 2, 2021 ya kuungua kwa sehemu ya kituo hicho ambacho kinasambaza umeme katika Mkoa wa Morogoro na maeneo mengine Nchini.

Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani kwa hatua alizozichukua za kuwasimamisha kazi wafanyakazi waliohusika na uzembe uliopelekea kituo hicho kuungua na kusababisha adha kwa watumiaji wa huduma ya umeme kutoka katika kituo hicho.

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri Dkt. Kalemani kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaobainika kuhusika na kuungua kwa kituo hicho pindi uchunguzi wa tume aliyoiunda utakapokamilika.

“Taarifa inaonesha kwamba kumbe ilisha onesha kuna hitilafu alafu mtu akalazimisha kuirudisha tena, ikaonesha tena ina shida na  bado akarudisha tena, mtu huyo ni mtaalam na anajua tatizo la umeme na anajua hatari ya umeme, Ni bora umemsimamisha kwa sababu amefanya makusudi” Alisema Mheshimiwa Majaliwa.

Awali akitoa taarifa ya Marekebisho katika kituo hicho, Waziri wa Nishati Dr. Medard Kalemani amelisema Wizara kwa kushirikiana na TANESCO pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa, Tayari wameagiza Transfoma yadharura ya Kilowati 30  kutoka Dodoma na  kuanzia jumatatu maeneo yote ya Morogoro yataanza kupata umeme wa uhakika.