Home Mchanganyiko KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE MAALUM AZINDUA MRADI WA MAJI NAMINYWILI-RUFIJI UNAOSIMAMIWA...

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE MAALUM AZINDUA MRADI WA MAJI NAMINYWILI-RUFIJI UNAOSIMAMIWA NA RUWASA

0

Kiongozi wa mbio za mwenge maalum wa uhuru,LT.Josephine Mwambashi akikagua na kutembelea miradi Wilayani Rufiji.(Picha na Mwamvua Mwinyi )

****************************

14, agost

Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
KIONGOZI wa mbio za mwenge maalum wa uhuru, LT.Josephine Mwambashi amekemea vitendo vya baadhi ya watu wanaoharibu miundombinu ya maji ,ambapo ameiasa jamii kulinda na kutunza vyanzo na miundombinu ya miradi ya maji.
Akizindua mradi wa maji Kijiji cha Nyaminywili , Rufiji mkoani Pwani,unaosimamiwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) na kukamilika kwa asilimia 100 kwa gharama ya milioni 195.358.2, Mwambashi alisema, maji ni uhai yapaswa kulinda miundombinu yake kwa manufaa ya jamii.
Alisema, serikali ya awamu sita ,inayoongozwa na Rais Samia Suluhu inajitahidi ili kila mwananchi afikiwe na huduma muhimu ikiwemo maji.
Mwambashi alifafanua, serikali imejipanga kwa kutenga fedha kutekeleza miradi ya maji ,mijini na vijijini ili kuondoa tatizo sugu la maji kwa kumtua ndoo mama kichwani.
“Wasimamizi wa miradi hii inapaswa nanyi muwe wazalendo na kuwashirikisha wananchi katika hatua za utekelezaji”alibainisha Mwambashi.
Hata hivyo , Mwambashi alielekeza RUWASA kuandaa taarifa ya kiasi cha sh.milioni mbili ambazo hazijawekwa katika taarifa ya mradi huo .
Awali akielezea,mradi huo ,meneja wa RUWASA Rufiji,Tluway Ninga alisema, makisio ya mradi huo yalikuwa milioni 257.543.3 , utekelezaji ulianza julai 2020 na kukamilika julai 2021.
Ninga alisema kuwa, mradi huo unasaidia wakazi 2,573 wa Nyaminywili kwa kupata huduma ya maji safi na salama.
Mkuu wa wilaya ya Rufiji,Meja Edward Gowelle alisema ,amepokea mwenge maalum wa uhuru agost 14 mwaka huu ukitokea Wilayani Kisarawe.
Meja Gowelle alielezea kwamba ,miradi sita itatembelewa na mbio za mwenge huo ,miradi yenye thamani ya sh.milioni 500.8 .
Mwenge ukiwa Rufiji pia umeweka jiwe la msingi katika ghala la mazao ya Kijiji cha Ndundunyikanza ,ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Ujamaa huko Ngorongo ,jiwe la msingi jengo la OPD zahanati ya Kijiji cha Mkongo.