Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kulia akimpa mkono na kumkabidhi madawati 60 mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Boko Timiza Fatma Pawa katika halfa iliyofanyika shuleni hapo na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali ambayo yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 ambazo zimetolewa na mfuko wa Jimbo.
Mbune wa Jimbo la Kibaha mjini wa kulia akiwa ameketi katika madawati ambayo ameyakabidhi na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ya msingi Boko Timiza iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha mkoani pwani ambayo yamenunuliwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kati kati aliyeshika mkasi akiwa anajiandaa kwa ajili ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kukabidhi madawati yapatayo 60 katika shule ya msingi book timiza ambayo yanunuliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo.
Afisa elimu msingi wa halmashauri ya mji Kibaha Bernadina Kahabuka akizungumza na kufafanua jambo katika ziara hiyo ya Mbunge yenye lengo la kuzitembelea shule za msingi na sekondari kwa ajili ya kuzikabidhi madawati.
Diwani wa Kata ya Tumbi Rymond Chokara akizungumza na viongozi mbali mbali wa halmashauri ya mji Kibaha pamoja na wajumbe wa mfuko wa jimbo wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka yenye lengo la kukabidhi madawati katika shule mbali mbali.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
*****************************
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu ameamua kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo kwa kuchangia madawati 220 katika shule tatu za sekondari na moja ya msingi zilizopo katika halmashauri hiyo ambayo yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilling milioni 12 ambazo zimetolewa kutoka katika mfuko wa Jimbo.
Koka alikabidhi madawati hayo kwa wakuu mbali mbali wa shule za sekondaari na msingi kwa ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa kwa wananchi sambamba na kutekeleza ilani ya chama ambapo amesema kwamba lengo lake kubwa ni kuweza kuwasaidia walimu na wanafunzi kuondokana na changamoto mbali mbali walizonazo.
Mbunge huyo amabye aliambatana na viongozi mbali mbali wa halmashauri ya mji Kibaha sambamba na baadhi ya wajumbe wa mfiuko huo wa jimbo alisema kwamba anatambua baadhi ya wanafunzi katika shule wanakabiliwa na kero kubwa ya kusoma wakiwa katika hali ya lundikano hiv yo ana imani sapoti hiyo ya madawati itaweza kuleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi kuweza kusomea katika mazingira ambayo ni rafiki.
“Katika ziara yangu hii lengo langu kubwa ni kutembelea katika baadhi ya shule za sekondari na msingi ikiwa ni kusapoti kwa namna moja hama nyingine sekta ya elimu na ndio maana kwa kutumia fedha za mfuko wangu wajimbo nimweza kutoa madawati hayo 220 katika shule mbali mbali na hii itaweza kuleta mabadiliko hata kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwani kwa sasa wataweza kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki,”alifafanua Koka.
Aidha Koka alisema moja ya mikakati yake ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na halmashauri ya mji Kibaha katika kuweka mipango madhubuti ambayo itaweza kuleta matokeo chanya katika kuboresha zaidi miundombinu ya madarasa, matundu ya vyoo sambamba na kuwajengea walimu miundombinu bora ya ofisi zao ili kuobgeza tija zaidi katika suala zima ya ufundishaji.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Tumbi Fidelis Haule alimpongeza Mbunge Koka kwa maamuzi yake ya kutoa sapoti ya madawati katika shule hiyo kwani hapo awali wanafunzi walikuwa wanakabiliwa na adha kubwa ya kusoma wakiwa wamekaa chini hivyo kwa msaasa huo utaweza kuwa ni chachu zaidi ya wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.
“Kwa upande wangu mimi kama mkuu wa Shule hii ya sekondari Tumbi napenda kutoa shukrani zangu za kipekee kwa Mbunge wetu wa jimbo la kibaha mjini kwa kuweza kutuona jinsi tulivyokuwa tunauhitaji mkubwa wa viti na mezi lakini kwa kuwa tumeshapatiwa viti vipatav yo 38 pamoja na meza zake 38 kwetu siis ni jambao jema sana katika kuwakomboa wanafunzi kutokukaa chini,”alisema Haule.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kihaba Robert Shilingi alisema kwamba anatambau mchango mkubwa ambao uanfanywa na mbunge koka katika suala zimala kusukuma gurugumu la maendeleo hususan katika nyaja ya elimu na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana naye kila kukicha ili kuweza kupiga hatua kwa shule za msingi na sekondari zilizopo katika halmashauri ya mji Kibaha.
Diwani wa kata ya Tumbi Rymond Chokara ambaye shule yake ya Msingi Boko Timiza imeweza kukabidhiwa jumla ya madawati 60 licha ya kutoa shukrani zake za dhati kwa Mbunge Koka kwa kuweza kufanikisha ahadi zake kwa vitendo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki na kwamba amemuomba ombi maalumu katika kata yake waanze mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ambayo itawaondolea adha wanafunzi ya kutembea umbari mrefu.
Afisa elimu msingi katika halmashauri ya mji Kibaha Bernardina Kahabuka alisema kwamba lengo la serikali ni kuendelea kusimamia sera ya elimu bure na kwamba wataendelea kumpa ushirikiano wa kutosha Mbunge huyo ili kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea na kuwaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika vikao mbali mbali vinavyoitishwa mashuleni lengo ikiwa ni kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Nao baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Picha ya ndege pamoja na shule ya sekondari kidimu na wao hawakusita kutoa shukrani zao kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji kwa kuweza kutenga fedha kupitia mfuko wa jimbo lake kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu na kuwasidia wanafunzi kuondokana na kilio chao cha kusoma katika hali ya mlundikano.
KATIKA ziara hiyo ya siku moja ambayo imefanywa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini aliweza kutembelea katika maeneo mbali mbali yanayohusiana na sekta ya elimu ambapo katika shule ya msingi Boko timiza aliweza kukabidhi madawati 60, shule ya sekondari tumbi viti na meza vipatavyo, 38, shule ya sekondari picha ya ndege viti na meza 20 ,pamoja na kukabidhi viti na meza 20 katika shule ya sekondari Kidimu.