Home Mchanganyiko BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA QATAR

BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA QATAR

0

******************************

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadili masuala ya kuimraisha uhusiano wa kidiplomasia, kuendeleza biashara na uwekezaji katika sekta za sekta za Madini, Utalii, pamoja na Mafuta na Gesi.