Home Mchanganyiko RC KUNENGE AHAMASISHA UWEKEZAJI ZAIDI KATIKA MKOA WA PWANI, ASEMA MKOA UNA...

RC KUNENGE AHAMASISHA UWEKEZAJI ZAIDI KATIKA MKOA WA PWANI, ASEMA MKOA UNA SIFA ZOTE ZA KUWEKEZA

0

 NA
MWANDISHI WETU.

MKUU
wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge amewaalika wawekezaji wa ndani na nje kwenda
mkoani humo kuwekeza kwenye eneo la viwanda kwani mkoa una sifa zote za
kuwekeza.

Alizitaja
sifa hizo kuwa ni pamoja na ardhi ya kutosha, usalama, kijiografia Pwani iko
katika enmeo lenye miundombinu ya kuwezesha bidhaa zizlizozalishwa viwandani
kufika kwa urahisi sehemu yoyote kwanin ni karibu na bandari lakini pia
miundombinu ya barabara nayo iko vizuri.

Mheshimiwa
Kunenge aliyasema hayo Agosti 3, 2021 wakati wa ziara ya kukagua kiwanda cha
kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar Ltd kinachomilikiwa na mwekezaji mzalendo
Said Salim Bakhresa.

Alisema
Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, imeshaweka wazi kuwa
wawekezaji waje kuwekeza nchini kwani serikali imeweka mazingira mazuri na
wezeshi ya kumfanya muwekezaji afaidike na uwekezaji wake.” Alisisitiza

Naye
mratibu wa mradi huo, Bw.  Sufian Ally,
Ameeleza kuwa  Serikali iliwapatia  Ekari 25,000
Mwaka 2016 na kwa awamu hii wamelima hekta 1330 na ifikapo Julai 2022
wataanza Kuzalisha sukari. Kazi za Ujenzi wa Kiwanda  zimekamilika kwa asilimia 95.

Ameeleza
kuwa kwa  awamu hii ya kwanza Kiwanda
kitatoa ajira kwa watu 1,500 na utakapo kamilika utaajiri watu 8,000.

Mhe.
Kunenge  amepongeza uwekezaji huo,
“Ni Uwekezaji Mzuri na sisi katika Mkoa wa Pwani ni mradi wa mfano na
miradi hii mikubwa kwa mkoa huu ni miradi yangu ninaifuatilia mwenyewe”
alisema Kunenge.