Home Uncategorized MAKATIBU WAKUU WA KAMATI YA FEDHA, UCHUMI NA BIASHARA WAKUTANA KATIKA KIKAO...

MAKATIBU WAKUU WA KAMATI YA FEDHA, UCHUMI NA BIASHARA WAKUTANA KATIKA KIKAO KAZI

0

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha , Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu chenye wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .  Kulia ni Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Ngelela Maganga. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 02/08/2021 katika Ukumbi wa Reform – uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Picha ikionyesha wajumbe wakifuatilia mjadala wa Kikao kazi cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika leo tarehe 02/08/2021 katika Ukumbi wa Reform – uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ngazi ya Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilika kwa kikao kazi cha Maandalizi ya Kikao cha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano. Katikati ni Mwenyekiti wa Kikao hicho Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango , Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba. Wengine katika picha, wa pili kutoka kulia ni Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na Bw. Amour Hamil Bakari, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Bi. Mary Ngelela Maganga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais na Bw. Khalid Hamrani Mkurugenzi, Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali – Zanzibar.