Home Mchanganyiko JAMII YAASWA KUWAJIBIKA KATIKA NGAZI ZOTE ILI KUTETEA NA KUENDELEZA UTARATIBU SAHIHI...

JAMII YAASWA KUWAJIBIKA KATIKA NGAZI ZOTE ILI KUTETEA NA KUENDELEZA UTARATIBU SAHIHI WA UNYONYESHAJI WATOTO MAZIWA YA MAMA

0

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Cosmas Nshenye akinywa uji wa Lishe wakati wa kufungua Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

***********************

Jamii imeaswa kuwajibika katika ngazi zote ili kutetea, kulinda na kuendeleza utaratibu sahihi wa unyonyeshaji watoto maziwa ya mama kwa kuwajengeza mazingira wezeshi kwa kina mama ili waweze kunyonyesha watoto maziwa ya mama.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Cosmas Nshenye kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani ambapo kitaifa yamezinduliwa mkoani Songwe na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa lishe ya watoto wachanga na wadogo.

“Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama ukifanyika ipaswavyo familia, jamii na taifa kwa ujumla watoto wachanga watakuwa na hali nzuri ya lishe itakayoboresha ukuaji na maendeleo yao kimwili na kiakili na kasi ya itapunguza vifo na kasi ya magonjwa ya kuambukizwa.” Amesema Mhe. Nshenye

Amesema kuwa twakimu za hali ya ulishaji watoto nchini Tanzania kwa mwaka 2018 zinaonyesha kuwa Tanzania imepiga hatua katika unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambapo 98% wanachagua kuwanyonyesha watoto wao, 92% watoto wanaendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee ndani ya miezi 6 ya mwanzo huku 87% ya watoto wanaanzishiwa vyakula vya nyongeza katika umri sahihi.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania TNFC Dkt. Germana Leyna amesema kuwa takribani vifo 823,000 vya watoto na 20,000 vya wanawake vinatokea wakati wa kujifungua duniani kila mwaka vinaweza kuzuiwa kutokana na unyonyeshaji na madhara ya kutonyonyesha maziwa ya mama kwa mtoto mchanga yanahusishwa na uwezo mdogo kiakili na kusababisha hasara za kiuchumi kwa kiasi cha dola bilioni 301 kwa mwaka.

Dkt Leyna anasema Tanzania imechukua jitihada mbalimbali za kulinda unyonyeshaji wa maziwa ya mama zikiwemo upitishwaji wa kanuni kuu 2 zinazolenga kulinda muda wa mama kuweza kunyonyesha na kumlinda mama na jamii, vilevile kutoa elimu kwa jamii yote ya watanzania ili itambue umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto.

“Jukumu kubwa la Taasisi ya Chakula na Lishe katika muktadha huu unyonyeshaji ni kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi za lishe ikiwemo suala zima la uhamasishaji maziwa ya mama kwa mtoto kupitia njia mbalimbali za upashaji habari”

Akitoa ushuhuda wa faida ya aliyoipata kwa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza Bi. Modesta Kayuni Mkazi wa kata ya Mlowo Mbozi mtoto hajawahi kuumwa tumbo kabisa na anakuwa na akili ambayo inaonekana iko vizuri na kushukuru wizara ya afya kwa kutuoa elimu ya umuhimu ya maziwa ya mama kwa mtoto mchanga.

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka huu2021 yamebebwa na kauli mbiu inayosema kulinda unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni jukumu letu sote.