Home Mchanganyiko GST NA NCAA ZAENDELEZA USHIRIKIANO WA KIKAZI

GST NA NCAA ZAENDELEZA USHIRIKIANO WA KIKAZI

0

***************************

Na.Samwel Mtuwa – GST.

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ( NCAA) katika utekelezaji wa kazi mbalimbali za Jiolojia.

Katika ushirikiano huo hivi karibuni GST kupitia mtaalam wake wa Jiolojia John Kalimenze imetoa mafunzo maalum kwa watumishi wa NCAA pamoja na wadau wa Utalii wa Jiolojia nchini yaani (Geoparks Stakeholders) juu ya usimamizi na uangalizi wa majanga ya asili ya jiolojia.

Mafunzo hayo yalifanyikia mkoani Arusha katika wilaya ya Karatu yalidhaminiwa na NCAA yakiwa na lengo la kujua sababu za majanga hayo kutokea , madhara yake kwa jamii na taifa kwa ujumla pamoja namna ya kujikinga na majanga hayo ya asili ya kijiolojia katika hatua tatu yaani kabla ya kutokea wakati yakitokea na baada ya kutokea.

Sambamba na mafunzo hayo GST imeshirikiana na NCAA katika kutambua vivutio vya Utalii wa Jiolojia yaani (Geosite for Geotourism) vinavyotambuliwa na Shirika la kimataifa la UNESCO lenye jukumu la kusimamia na kuangalia vivutio vya Utalii wa Jiolojia duniani.