Home Mchanganyiko MRISHO MPOTO, BARNARBA BOY NA FREDY KANO WAUNGA MKONO KAMPENI YA CHANJO...

MRISHO MPOTO, BARNARBA BOY NA FREDY KANO WAUNGA MKONO KAMPENI YA CHANJO YA CORONA

0

Mwanamuziki Mrisho Mpoto akionesha cheti chake cha kuchanja chanjo ya UVIKO 19 wakati yeye na msanii mwezake Barnarba Boy na Freddy Kano walipozindua wimbo wao wa “Mama Hawezi Muuza Mwanawe ili  kuhamasisha wananchi kuchanja chanjo hiyo.

Mwanamuziki Mrisho Mpoto na msanii mwezake Barnarba Boy wakizindua  wimbo wao wa “Mama Hawezi Muuza Mwanawe ili  kuhamasisha wananchi kuchanja chanjo hiyo.

……………………………………

Wasanii wa muziki Mrisho Mpoto, Barnaba Boy na Felly Kano wamezindua wimbo wao mpya ujulikanao kama “Twendeni tukachanje, Mama hawezi Muuza Mwanawe” wenye lengo la kuhamasisha Jamii kuchanja kwa ajili ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona.

Wimbo huo mpya wa sauti na video umetolewa bure kwa Jamii ambapo mtu yoyote anaweza kuutumia kwa namna yoyote ya kutoa elimu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wimbo huo, msanii Mpoto amesema kutokana na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha analinda Watanzania dhidi ya janga la Virusi vya Corona (UVIKO-19).

“Tumeona juhudi za Rais Wetu Samia Suluhu Hassan, nasi kwa kutumia nafasi yetu tumeamua kumuunga mkono” amesema Mpoto.

Nae Barnaba Boy amesema ipo haja kwa Jamii yote kupata chanjo ya Corona ili kujikinga na Ugonjwa huo na kwamba wao kama wasanii tayari wameshaonesha mfano kwa kuungana na Rais kwenye zoezi hilo lililozinduliwa Julai 28 mwaka huu.