Home Mchanganyiko DIWANI LIDYA MGAYA -CHANJO YA UVIKO 19 NI MOJA YA MAPAMBANO YA...

DIWANI LIDYA MGAYA -CHANJO YA UVIKO 19 NI MOJA YA MAPAMBANO YA KUUTOKOMEZA UGONJWA HUO

0
………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Diwani wa Viti Maalumu Kibaha Mjini ,Lidya Mgaya amesema chanjo ya UVIKO 19  ni mapambano tosha ya kudhibiti ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kujikinga kwa barakoa na kunawa maji tiririka.
Ametoa pongezi kwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuzindua hatua ya Kisayansi ya kupambana na homa kali ya Mapafu UVIKO 19 kwa kutumia njia ya Chanjo.
Lydia alieleza hayo mara baada ya yeye kupata Chanjo ya UVIKO-19 leo Kibaha Mjini. 
Lydia ameeleza kuwa Pamoja na chanjo hiyo kuwekwa katika Hiari ya Mtu lakini  ni vema watanzania kujitokeza kuunga juhudi hiyo ya kisayansi kwani yeye binafsi akiwa kama mama wa watoto wanne ambao wote aliwapatia chanjo za kupambambana na maradhi mbalimbali nakuona faida yake, hivyo atakuwa mstari wa Mbele kujitokeza kwenda kuchanja ili kuendeleza Mapambano ya UVIKO-19.
“ Nimefurahi sana Kupata chanjo ya UVIKO-19 hapa Kibaha Mjini Baaada ya Kupewa Taarifa na Mwenyekiti wangu wa UWT Wa Mkoa wa Pwani, nimefurahi sana kupokea Chanjo nikiwa na Mume wangu ambaye yeye atapokea Chanjo katika Kituo Cha Lugalo Kesho” alisema Lydia
Aidha Lydia amempongeza , Rais Samia kwa kuongoza kwa vitendo kwa yeye binafsi Kuchanja ikiwa ni kuonyesha watanzania kuwa sasa tunatumia silaha nyingine ya Mapambano ya UVIKO-19 ya kisayansi ili kuendelea kupambana na Homa hiyo kali ya Mapafu.
Anawashauri watanzania kutumia uhiari wao katika kufanya maamuzi sahihi katika hatua hii ya kisayansi iliyoanzishwa ya kupambana na UVIKO-19 ili jamii yetu ya Tanzania iendelee kubaki Salama Zaidi.
*Corona Inazuilika Jikinge Uwakinge Wengine*