Home Siasa WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU MOROGORO WARIDHISHWA NA UJENZI WA RELI YA KISASA...

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU MOROGORO WARIDHISHWA NA UJENZI WA RELI YA KISASA DAR HADI MOROGORO.

0

…………………………………………………………….
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)Mkoa wa Morogoro imetembelea mradi wa kimkakati wa reli ya kisasa(SGR) kutoka Kihonda Manispaa ya Morogoro hadi Kilosa ambapo imeonyesha kulidhishwa na kazi iliyofanywa na mkandarasi chini ya shirika la reli nchini TRC.
Mara baada ya kutembelea na kujionea mradi huo wajumbe hao wamempongeza Rais wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania Mhe Samia Suruhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchi ambayo iliamzishwa na hayati Dkt. John Magufuli.
Akizungumza mara baada ya kujionea maendeleo ya mradi huo wa reli ya SGR Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku alisema chama kimefanya kazi kubwa katika kusimamia miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa kupitia ilani ya CCM.
Mwamsiku alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo utasaidia upatiakanaji wa ajira kwa vijana pamoja na kinamama na kuondokana na wimbi la umasikini ambalo limesababisha vijana wengi kuingia katika makundi yasiofaa na kukosa uzalendo na nchi yao.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mradi huo utakuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa Mkoa wa Morgoro kwani utakapokamilika utarahisisha ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa mikoa ya Dar Es Salaam na Morogoro.
“Kukamilika kwa mradi huu utatufanya sisi wana CCM kutembea kifua mbele zaidi tunapoenda kwa wananchi kuomba kura kwani ilani ya chama itakuwa imetekeleza kikamilifu.”alisema Mwenyekiti wa CCM.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigela alieleza namna Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suruhu Hassani inavyosimamia kwa weledi miradi ya kimkakati ikiwemO reli ya SGR unaopita katika Mkoa wa Morogoro na unavyonufaisha wananchi huo.
Alisema mradi huo umewapatia vijana na wanawake ajira na kuinua uchumi wao kwa kupia nyacha mbalimbali ikiwemo katika Ulinzi, ujenzi huku wanawake wakijipatia fulsa ya kuuza chakula (mama lishe) kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika ujenzi huo.
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Martin Shigela alilipongeza shirika la reli Tanzania TRC kwa kazi kubwa linaloifaifanya katika kusimamia mradi wa kisasa ambao Taifa linauangalia kwa jicho la tatu kwani kukamilika kwa mardi huo kuitaifanya Tanzania kuingia katika nchi zenye miundombinu bora ya duniani.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kilosa na Waziri wa katiba na sharia Profesa Palamagamba Kabudi aliwataka watanzania kuacha kukosoa kila kitu kinachofanywa na serikali badala yake wawe mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi na mafanikio yanayofikiwa na Taifa ikiwemo ni pamoja na utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati.
Akizungumza mara baada ya kutembea mradi wa SGR Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Morogoro Alexia Kamguna aliiomba serikali kuwapa nafasi wafanyabiashara wadogo hususani wanawake kwenye maeneo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa hapa nchini.
“Niiombe tu serkali kwenye hizi stesheni pia mngetenga sehemu kwa ajili ya wanawake kuja kuuza bidhaa zao ndogondogo hapa ingewapa fulsa nao kujiingizia kipato kuliko kutenga maeneo ya biashara kwa ajili ya wafanyabiashara wakubwa tu.”alisema Kamguna.
Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Maselle alisema watanzania wanatakiwa kujivunia mradi huu ambao unatekelezwa kwa fedha za watanzania jambo ambalo linatia faraja kwa watanzania,huku akiwataka watembee kifua mbele.
Awali akitoa maelezo kwa viongozi wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)Mkoa wa Morogoro Meneja MradiMradi msimamizi kipande cha Dar es salaam na Morogorogo kutoka shirika la reli Tanzania TRC Thadey Paul alisema mardi huo utaanza kufanyiwa majalibia mwezi wa 11 ambapo majalibia hayo yatafanywa ndani ya miezi mitatu.
Halmshauri hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku ilitembelea stesheni ya reli ya SGR iliyopo Kihonda na maeneo mengine ambayo ujenzi unaendealea.