Home Michezo TANZANIA MABINGWA CECAFA

TANZANIA MABINGWA CECAFA

0

****************************

Timu ya Taifa ya Tanzania Vijana wenye umri chini ya miaka 23 wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya CECAFA Challenge CUP kwa kuifunga timu ya taifa ya Burundi kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mechi hiyo kuisha kwa 0-0 ndani ya dakika 90.

Fainali hiyo ambayo ilipigwa katika dimba la Bahir Dar nchini Ethiopia tulishuhudia timu zote zikihitaji ushindi ndani ya dakika 90 bila mafanikio.

Tanzania iliingia fainali baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Sudani Kusini bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali akati Burundi alipata nafasi ya kuingia fainali baada ya kumfunga Kenya.