Home Michezo MO DEWJI AWEKEZA BILIONI 20 KWENYE KLABU YA SIMBA SC

MO DEWJI AWEKEZA BILIONI 20 KWENYE KLABU YA SIMBA SC

0

*****************************

Mwenyekiti wa Bodi wa Klabu ya Simba Sc Mohammed Dewji leo ameweka hisa ya asiilimia 49 yaani Shilingi Bilioni 20 kwenye klabu hiyo kama mdhamini wa klabu ili kuwezesha klabu hiyo kufanya vizuri kwenye soka na kuweza kufika mbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mo Dewji ameomba taasisi hiyo iendeshwe kwa uwazi na kwa nidhamu na asitokee mtu au kikundi cha watu kufanya kitu ambacho kitaigharimu timu hiyo.

“Naomba hii Taasisi iendeshwe kwa uwazi na kwa nidhamu ya hali ya juu hatuwezi kutoka kwenye ishu ya nidhamu, la tatu hakuna Mtu mkubwa kuliko Simba, Simba tumeikuta, sisi tutakufa tutaiacha Simba itaendelea, hatuwezi kukubali Mtu kuwa juu ya Simba na hiyo hata Mimi ‘Mo’ sio mkubwa kuliko Simba”. Amesema Mo Dewji.

Amesema ndani ya miaka minne ametumia kiasi cha shilingi Bilioni 21.3 ambapo Bilioni 5.3 ilitumika kusajili wachezaji, makocha,pre season, mishahara na uendeshaji wa klabu hiyo.

Pamoja na hayo Mo dewji amesema kuwa wameshakamilisha mchakato wa mabadiliko ambapo wamepata hati kutoka tume ya Ushindani (FCC) ya kuwaruhusu kumaliza mchakato.