Home Burudani BEN POL AJA Na KIFURUSHI CHA “B”

BEN POL AJA Na KIFURUSHI CHA “B”

0

…………………………………………………………..

Msanii wa Muziki wa Miondoko ya R n B nchini Behnam Paul maarufu kama Ben Pol amewazawadia mashabiki zake kifurushi chenye nyimbo Nne mpya (4) alichokiita “B”.

Ben Pol ameachia nyimbo hizo leo ambapo mojawapo amemshirikisha Msanii Billinas aliyoiita Kisebusebu, nyingine ni Unaita, For You na Warira ambayo tayari alishaiachia mapema mwezi huu.

Msanii huyo amesema, ameamua kuita B kwa sababu inabeba stori na hali tofauti tofauti katika mapenzi kupitia nyimbo hizo nne.

“Naamini jumbe zitaeleweka kwa watu wengi kwa kuwa ni mambo ambayo tunayaishi kila siku,
Upendo ndio jibu, na muziki ndio njia, nami namshukuru kila mmoja kwa Upendo na support yake kwangu” amesema Ben Pol

Amesema kuwa bado anaendelea kuwashukuru mashabiki wake kwa kupokea nyimbo na kuendelea kufanya vizuri na amewaahidi kuendelea kuwapa ladha tofauti kila siku.

B inapatikana katika mitandao yote ya muziki na vituo vya redio ndani na nje ya nchi.

Nyimbo hizo zimetayarishwa katika studio za Pizzey Records na watayarishaji Chatta, O.righty na Jaco Beatz.