Home Michezo KOCHA WA YANGA NASREDDINE NABI AWABWAGA GOMES WA SIMBA NA LULLE WA...

KOCHA WA YANGA NASREDDINE NABI AWABWAGA GOMES WA SIMBA NA LULLE WA MBEYA CITY NA KUTWAA TUZO KOCHA BORA WA LIGI KUU JULAI

0

Kocha Mkuu wa Yanga  Nasreddine Nabi ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu kwa mwezi wa mwisho wa msimu, Julai baada ya kuwashinda Mfaransa Didier Gomes wa Simba na Mganda, Mathias Lulle wa Mbeya City.
Nabi aliiongoza Yanga kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza mwezi huo, 1-0 dhidi ya mabingwa, Simba na 2-0 dhidi ya Ihefu huku mwingine ikitoa sare ya 0-0 na Dodoma Jiji FC.