Home Biashara MSHINDI WA PROMOSHENI YA BIA YA BALIMI AKABIDHIWA ZAWADI YA POWER TILLER

MSHINDI WA PROMOSHENI YA BIA YA BALIMI AKABIDHIWA ZAWADI YA POWER TILLER

0

Mshindi wa Power Tiller kupitia  promosheni ya  bia ya Balimi Maclina Romward Rugeiyamu akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa zawadi yake,wengine pichani ni Maofisa wa kampuni ya TBL, Hafla ya kumkabidhi ilifanyika mjini Bukoba mwishoni mwa wiki.

Maclina Romward Rugeiyamu (wa kwanza kulia) mkazi wa Bukoba mkoani Kagera akifurahia zawadi ya Power Tiller aliyojishindia kupitia promosheni ya bia ya Balimi baada ya kukabidhiwa na Meneja wa bia hiyo,Pamela Kikuli (katikati) wengine pichani ni Maofisa Mauzo wa TBL.Hafla ya kumkabidhi ilifanyika mjini Bukoba mwishoni mwa wiki.

***************************

Mkazi wa Bukoba mkoani Kagera, Maclina Romward Rugeiyamu, mwishoni  mwa wiki alikabidhiwa zawadi ya jembe la kutumia teknolojia ya kisasa (Power Tiller) alilojishindia kupitia promosheni inayoendelea ya bia ya Balimi  Extra Lager.

 

Promosheni hiyo ya wiki nane iliyozinduliwa mwezi uliopita inawezesha  wateja wa bia ya Balimi kujishindia Power Tiller, muda wa maongezi, bia za bure, na T-shirts.

 

Meneja wa bia ya Balimi,Pamela Kikuli akiongea wakati wa hafla hiyo,aliwataka wakazi wa kanda ya ziwa ambako promosheni hiyo inafanyika kuendelea kunywa ya Balimi na kutuma tarakimu watakazozikuta chini ya kizibo kwenda namba 15054 ambapo zitaingizwa kwenye droo ya wiki inayofanyika kupitia luninga ya Star .“ Bado kuna power tiller sita hazijapata washindi na zawadi nyingi za vocha za muda wa maongezi,hivyo wateja wenu wanayo fursa ya kuchangamkia zawadi hizi”alisema.

 

Naye Maclina Rugeiyamu alitoa shukrani kwa kampuni ya TBL kwa kubuni promosheni zenye malengo ya kunufaisha weateja wake “Zawadi hii itaniwezesha kuendesha kilimo cha kisasa kitakachowezesha kujiongezea kipato na kuboresha maisha yangu na familia.