Home Mchanganyiko KUSAMBAA KWA TAARIFA ZA ASKARI KUINGIA KANISA LA MWANJELWA – KINYUME CHA...

KUSAMBAA KWA TAARIFA ZA ASKARI KUINGIA KANISA LA MWANJELWA – KINYUME CHA SHERIA.

0

******************************

Mnamo tarehe 25/07/2021 tumeona tarifa zikisambaa kwenye mitandao mbalimbali kwamba Askari Polisi wakiwa na Silaha wameingia katika Kanisa Katoliki la Mwanjelwa kuwakamata Waumini waliokuwa wamevaa sare za CHADEMA kinyume cha sheria.

Polisi Mkoa wa Mbeya tunaendelea kusimamia Ulinzi na usalama wa Raia na mali zao na suala la doria na patrol za miguu na Magari huwa linafanyika kila siku wakati wa mchana na usiku.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa vikundi vyote vya kijamii au vyama vya Siasa pindi wanapotaka kufanya jambo Iolote ambalo litawahusisha wengine kufanya mawasilaano na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya tunakanusha uvumi unaoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna Askari Polisi waliohusika kuingia Kanisani na kuwakamata waamini waliovalia mavazi ya CHADEMA wakati ibada inaendelea.