Home Mchanganyiko WAZIRI BASHUNGWA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KARAGWE

WAZIRI BASHUNGWA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KARAGWE

0

Mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akiwa ameambatana na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Karagwe, Mwenyekiti na Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi Karagwe wakiwa kwenye boti ya Mv. Ruhita wakielekea katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto katika vijiji vya Mirilo, Kigasha na Chamengo vilivyopo ngambo ya ziwa Burigi wilaya ya Karagwe, Julai 21, 2021

Mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akiwa katika mkutano wa kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto katika vijiji vya Mirilo, Kigasha na Chamengo vilivyopo ngambo ya ziwa Burigi kata ya Rugu wilaya ya Karagwe, Julai 21, 2021

********************************

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa Serikali kupitia mfuko wa Jimbo na fedha za halmashari ambazo zitatengwa kwa ajiri ya miradi ya maendeleo kuimalisha miundombinu ya elimu, afya na Barabara katika vijiji na vitongoji ambavyo vipo ng’ambo ya ziwa na vijiji ambayo vimekuwa ni vigumu kufikika katika Jimbo la Karagwe.

 

Waziri Bashungwa ameyasema hayo Julai 21, 2021 alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali katika vitongoji vya Mirilo, Chamengo na Kigasha katika Kijiji cha Ruhita kata ya Rugu wilaya ya Karagwe vilivyopo ngambo ya Ziwa Burigi.

Wakati akijibu changamoto katika vitongoji hivyo, Bashungwa ameeleza kuwa barabara za ambazo zimekuwa zikipitika kwa shida wakati wa mvua za Rugera kwenda kigasha na Mirilo zitafanyiwa ukarabati ili kufungua uchumi wa vitogoji hivyo ambavyo vipo ngambo ya ziwa, hivyo hivvyo kwa upande wa changamoto ya maji wakati wa kiangazi ameeleza kuwa RUWASA itafika katika Kijiji hicho ili kutembelea chanzo cha maji Rwenyangira ili iweze kutengwa bajeti ya kukarabati ili wananchi wapate maji safi na salama.

Aidha, Kwa changamoto ya umeme kutofika katika vitongoji vyote ameeleza kuwa Serikali ipo mbioni kusambaza umeme katika maeneo yote nchini hivyo hata kwenye vijiji hivyo atahakikisha havisahauliki katika awamu hiyo ya usamabazaji wa umeme.

Nae, Diwani wa Kata ya Rugu, Bw. Adrian Kobushoke ameshukuru Serikali kupitia Mbunge wa Jimbo la Karagwe kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya ya kusukuma miradi ya maendeleo ambayo imekuwa ikitekelezwa katika kata hiyo hasa kwa ujenzi wa shule ya msingi Miliro ambayo imepata usajili mwezi wa tatu mwaka huu ambapo kwa sasa vyumba sita vya madarasa vimejengwa, ofisi ya walimu, stoo na matundu nane ya vyoo.