Home Siasa TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE VITI MAALUM 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE VITI MAALUM 

0

…………………………………………………………………….

Dodoma 

Kwa mujibu wa kifungu cha 86A (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kikisomwa pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 na kifungu cha 19 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake kilichofanyika tarehe 20 Julai, 2021 imewateua Madiwani Wanawake Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kama ifuatavyo; 

(i) Ndugu Kaduma Magreth Abisai kuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe; 

(ii) Ndugu Victoria Batendi Ndaki kuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

(iii) Ndugu Rhoida Andrea Chengula kuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. 

Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 (1) (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, imefanya uteuzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ikiitaarifu Tume juu ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani Wanawake wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kutokana na kifo cha Bi. Mwamini John Wikesi, Halmashauri ya Wilaya ya Geita kutokana na kifo cha Bi. Rehema Omary Manangwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kutokana na kifo cha Bi. Theresia Pebro Kiswaga.