Kaimu Katibu
Tawala Upande wa Elimu Mkoa wa Tanga na Zalia Gaula akizungumza wakati
wa Maonyesho ya Sayansi kwa Vijana wa Shule za Sekondari Mkoani
Tanga yamefanyika kwa mara ya kwanza katika shule ya Sekondari Tanga
School
Afisa Elimu Upande wa Sekondari Jiji la Tanga
Lusajo Gwakisa akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mratibu wa Young Scientist Tanzania Tanga Nelson Makundi akizungumza
Sehemu ya Walimu wakifuatilia maonyesho hayo
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja |
MAONYESHO ya Sayansi kwa Vijana wa Shule za Sekondari Mkoani
Tanga yamefanyika kwa mara ya kwanza huku wanafunzi walionyesha ubunifu
mbalimbali na kuweza kusaidia kupambana na changamoto zilizopo kwenye ulimwengu
wa sasa kwa kutumia Teknolojia na Sayansi.
Akizungumza wakati wa maonyesho hayo kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi ,Mratibu wa maonyesho hayo ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za
Sekondari Mkoa wa Tanga Mwalimu Nelson Makundi alisema lengo kubwa la la
maonyesho hayo ni kutumia Sayansi na Teknolojia kuibadili Tanzania ya sasa
Alisema kutokana na kwamba sayansi ikitumika vizuri inaweza
kuwa chachu ya kuweza kufikia maendeleo makubwa kutokana na kwamba hata viwanda
ambavyo vitaanzishwa vitahitaji wataalamu ambao wataweza kufanya shughuli
kwenye maeneo hayo.
“Nitoe wito kwa Serikali kwani maonyesho hayo yamekuwa
yakifadhiliwa na wafadhili mbalimbali lakini walikuwa wanatama sana wao nao
wawaunge mkono kwa sababu Taifa
linategemea sana sayansi kwa maendeleo”Alisema
Hata hivyo alisema upo umuhimu wa Serikali kuunga mkono
juhudi zote zinazofanywa na wanasayansi na vijana hao ili kuweza kufanikisha
malengo kwa Taifa na kuifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri ya kuishi.
Awali akizungumza wakati wa maonyesho hayo Kaimu Katibu
Tawala Upande wa Elimu Mkoa wa Tanga na Zalia Gaula alimpongeza Mkuu wa Shule
ya Sekondari Tanga School Andrew Mwakanyamale kwa kupatia nafasi ya kuweza kuandaa
mashindano hayo ambayo yamefanikiwa sana ikiwemo walimu ambao walijitoa pamoja
na vipindi vya kawaida kuweza kuwasaidia wanafunzi hao.
Alisema amepitia kwenye maonyesho hayo ni mazuri kutokana na
kila mwanafunzi kuwefanya kazi nzuri sana huku akiwataka kuhakikisha wanapokuwa
madarasani wana kuwa makini kusikiliza walimu wenu wanachokifundisha ili waweze
kukitumia kwenye kupata ufaulu.
“Mwanasayansi mkubwa anaanzia kwenye maonyesho kama hayo hivi
sasa Tanzania tumeingia kwenye uchumi wa Kati wa viwanda ambapo tunahitaji
wanasayansi na wanasayansi wanatengenezwa hivyo sisi kama mkoa tunaouwezo wa kuwaandaa wanayansi
baadae wakawa na mchango mkubwa kwenye Taifa ”Alisema
Alisema pia amefurahishwa na kifaa cha kuzuia mawasiliano
kwa sababu kama mwanafunzi anatumia simu bwenini inamzuia hivyo wamefanya kitu
kizuri kutokana na kwamba shule nyingi
zinaunga moto lakini wanasema chanzo hakujiukalani lakini tatizo kubwa ni njia za
kuchaji simu ambapo wanafunzi wanatafuta sehemu ya kuchagi simu ivyo
wanaunganisha nyaja bila kuwa na ujuzi.
Afisa Elimu Taaluma hiyo alisema hatua hiyo inapelekea
mabweni kushika moto na hivyo ni kuzuri huku akitaka nitakapoanza kufanya kazi
ni vizuri kianze kutumika kwenye shule hiyo .
Hata hivyo aliwashauri wakuu wa shule,walimu na walezi wapate muda ya kukaa na wanafunzi wenye
changamoto za kujirudia mara kwa mara kwani makosa hayo ndio yanasababisha
wasifanye vziuri darasani hivyo wanaweza kukuta wanafunzi wenye matatizo ya
kifamilia.
Alisema hivyo ni muhimu kuona namna nzuri ya kuwasaidia ili
kuweza kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao ikiwemo kueleza kuvutiwa na maonyesho
hayo kwa sababu wametumia dhana na vifaa vinavypatikana kwenye maziingira ya
hapa nchini.
“Lakini natamani siku moja kwa hicho wanachofanya wanafuzi
wanaweza kutafuta chanzo cha kufanya njia mbadala ya asili ya kutumia mmea au
kitu ambacho kitaweza kutumika kufukukuza mbu waonekeza malaria maana ugonjwa
huo ni hatari”Alisema
Kwa upande wake Afisa Elimu Upande wa Sekondar Jiji la Tanga
Lusajo Gwakisa alisifu juhudi ambazo zimeonyeshwa kwenye uandaaji wa maonyesho
hayo huku akitoa ombi lake kwa wanafunzi wa sayansi na masomo mwengine kuendelea
kujitahidi na kuzingatia wanayofundishwa walimu.
“Kwa maana wanajitahidi nimefurahi kuona watoto wanajua
kufanya utafiti na kukusanya data na kufanya uchambuzi wa data na kilichoni
furahisha ni ubunifu mkubwa mliokuwa mkiunyesha niwaombe wote mjitahidi mfike
Chuo Kikuu”Alisema
Hata hivyo alisema angeomba wale ambao wamejitahidi kuendelea
kufanya vizuri na wao kama Halmashauri Idara ya Elimu sekondari watawasaidia mazoezi
yote yalikuwa yakiendeshwa kwa kukosa vifaa na masuala mengine kwa wale wote
waliofanya wataboresha zaidi.