Home Mchanganyiko TAHLISO YAITAKA BODI YA MIKOPO KUWALIPA MAPEMA WANAFUNZI FEDHA ZA (FIELD) MASOMO...

TAHLISO YAITAKA BODI YA MIKOPO KUWALIPA MAPEMA WANAFUNZI FEDHA ZA (FIELD) MASOMO KWA VITENDO

0

Rais wa Shirikisho la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini(TAHLISO) Bw. Frank Nkinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es salaam kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu bodi ya mikopo kwa wanafunzi.

Baadhi ya viongozi wa TAHLISO waliohudhuria katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.

Viongozi wa Shirikisho  la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini(TAHLISO) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo.

……………………………………….

SHIRIKISHO la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini(TAHLISO) ameitaka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL), kutoa fedha kwa wanafunzi wanaopaswa kwenda masomo ya vitendo (Field).

Amesema tangu wiki iliyopita baadhi ya wanafunzi wameanza kwenda kujifunza kwa vitendo lakini bado hawajapewa fedha za kujikimu na HESBL.

Mwenyikiti wa TAHLISO, Frank Nkinda, ameyaeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo maslahi ya taifa.

“Tunaomba Rais Samia, atusaidie fedha hizi zitoke mapema ili wanafunzi waweze kwenda field kwa wakati,” alisema Nkinda.

Sambamba na hilo, alimshukuru Rais Samia kwa kuona umuhimu wa wanafunzi kuendelea kupata mikopo kwa kuongeza kiwango kutoka Sh. milioni 464 hadi Sh. bilioni 570.

Kadhalika aliishukuru serikali kwa kuondoa riba ya asilimia sita kwenye mikopo ya wanafunzi waliohitimu elimu ya juu.

“Kwa bahati nzuri Rais amesikia kilio chetu kwa kuondoa tozo hii kwa sababu ilikuwa ni mwiba kwa wahitimu wa elimu ya vyuo vikuuu nchini,” alisema Nkinda.

Amesema Serikali imejenga miundombinu kuwawezesha wanafunzi kupata elimu lakini bado wasomi na vijana wa taifa hawajaweza kutafuta mbinu za kutatua changamoto za ajira.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kusikia kilio cha Watanzania na kuahidi kutatua kero ya tozo za miamala.

Alisema maagizo yaliyotolewa na Rais Samia yanatosha kumshukuru kwa kusikia kilio cha Watanzania wengi ambao wameumizwa na tozo hizo zilizoanza kukatwa hivi karibuni.