Home Michezo SIMBA SC YAKABIDHIWA KOMBE LAO, YAICHAPA NAMUNGO FC MABAO 4-0

SIMBA SC YAKABIDHIWA KOMBE LAO, YAICHAPA NAMUNGO FC MABAO 4-0

0

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba SC imefanikiwa kuichapa Namungo Fc mabao 4-0 kwenye mchezo wa mwisho wa ligi kuu bara mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba Sc katika mchezo wa leo wamekabidhiwa kombe lao la ligi baada ya kuwa mabingwa wa ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 83 katika michezo 34 huku mahasimu wao Yanga wakishika nafasiĀ  ya pili wakiwa na pointi 74.

Mabao ya Simba yaliwekwa kimyabi na Mshambuliaji wao Meddie Kagere dakika 19 ya mchezo kipindi cha kwanza na bao la pililikifungwa Chris Mugalu ambaye alifunga mabao mawili mnamo dakika ya 24 na dakika ya 67.

Nahodha wa klabu hiyo John Bocco aliingia kipindi cha pili na kuweza kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penati dakika ya 94 na kumuwezesha kuibuka kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo ambayo ilikuwa yakuvutia.