Mkurugenzi wa shule ya msingi na sekondari Joyland zilizoko Toangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, Fredrick Okuku akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa mbio za marathoni kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika leo.
Wanafunzi wa shule ya awali Joyland ya Toangoma Kigamboni wa Simba na Yanga wakipambana kwenye soka wakati wa Bonanza la Michezo la shule hiyo leo kwenye viwanja vya shule hiyo.
Mkurugenzi wa shule ya msingi na sekondari Joyland zilizoko Toangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, Fredrick Okuku akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa mbio za marathoni kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika leo.
Wanafunzi wa Green House wa shule ya Joyland wakishuhudia michezo mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika leo kwenye viwanja vya shule hiyo Toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Blue House wa shule ya Kimataifa ya Joyland ya Toangoma wakishuhudia michezo mbalimbali iliyokuwa ikiendelea kwenye Bonanza la shule hiyo lililofanyika leo kwenye viwanja vya shule hiyo Toangoma Kigamboni Dar es Salaam.
**********************
Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI wa Shule ya Kimataifa ya Joyland ya Toanganoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, wametia fora kwenye bonanza ambapo wameonyesha vipaji vya aina mbalimbali.
Katika bonanza hilo lililowashirikisha wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari Joyland, wanafunzi hao walionyesha umahiri kwenye kuigiza michezo mbalimbali ikiwemo ile kushindana kula haraka.
Miongoni mwa vitu vilivyotia fora kwenye bonanza hilo ni mbio fupi na ndefu, kukimbia na magunia, kuruka viunzi na namna walivyomudu kuwasilisha sanaa hiyo kwa ubunifu mkubwa.
Mwalimu wa michezo wa shule hiyo, Jonathan Mbogoma, alisema alisema waliandaa bonanza hilo kwaajili ya kuendeleza vipaji vya wanafunzi hao kwenye fani mbalimbali na kwamba hufanyika mara tatu kila mwaka.
Alisema mbali na masomo ya darasani shule imeona umuhimu wa kuwakutanisha wanafunzi hao kwenye bonanza ili waonyeshe vipaji walivyonavyo kwenye mitindo ya mavazi, muziki wa bongo fleva na maonyesho ya mitindo ya mavazi.
Alisema watakuwa wakiandaa bonanza kama hilo mara kwa mara kwaajili ya kuvumbua vipaji na kuvilea kwani vinaweza kukua na kuwanufaisha kwenye maisha yao ya baadaye.
“Mbali na masomo ya darasani tumeona kuna umuhimu wa kubaini vipaji vya wanafunzi na kuvikuza mtoto lazima alelewe katika nyanja mbalimbali kwasababu mwisho wa siku anawez kuishi kutegemee kipaji chake,” alisema
“Kuna mifano ya wanamuziki wengi ambao wamefanikiwa sana kwenye maisha kutokana na vipaji mbalimbali, mwanafunzi anaweza asifanye vizuri sana darasani lakini akawa na kipaji kitakachompa maisha mazuri sana,” alisema.
Alisema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2015 imekuwa iithamini michezo kwa kufanya mabonanza kama hayo kila mwaka kusaka vipaji.