Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (kulia) akieleza kuhusu umuhimu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, kuongeza ushirikiano kwa Serikali ya Zanzibar, ili kufanikisha utekelezaji wa Sera za Fedha, wakati alipotembelea BoT tawi la Zanzibar, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo visiwani Zanzibar, kushoto ni Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Bernard Kibesse.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) na Viongozi wa BoT tawi la Zanzibar, katika ukumbi wa BoT Zanzibar.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) akiongoza mkutano kati yake na viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, alipotembelea tawi hilo, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo visiwani Zanzibar.
Mkurungenzi Ofisi Ndogo ya BoT- Zanzibar, Dkt. Camillius Kombe, akielezea Sera ya Fedha inavyozingatia hali ya uchumi wa Visiwa vya Zanzibar, wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) na viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar,
Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, Bi. Dyness Francis Mdoe, akielezea jambo, wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) na viongozi wa BoT katika tawi hilo, visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (kushoto) na Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Bernard Kibesse, wakiteta jambo, alipowasili katika Ofisi Ndogo za Benki hiyo, tawi la Zanzibar, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo visiwani Zanzibar.
Afisa Tiba wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, Dkt. Ibrahim Mgao, akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa Benki hiyo katika kukuza uchumi wa Zanzibar, wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) na viongozi wa BoT katika tawi hilo, visiwani Zanzibar.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse, akimuongoza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (katikati) alipokuwa akiondoka katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Zanzibar, baada ya kufanya mkutano na viongozi wa Benki hiyo, visiwani Zanzibar. Kulia ni Mkurungenzi Ofisi Ndogo ya BoT- Zanzibar, Dkt. Camillius Kombe.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (katikati), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse (kushoto) na Mkurungenzi Ofisi Ndogo ya BoT- Zanzibar, Dkt. Camillius Kombe, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BoT tawi la Zanzibar.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Yussuf Masauni (Mb) (wa pili kushoto) akisalimiana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Bernard Kibesse, alipowasili Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Zanzibar, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, visiwani Zanzibar
(Picha na Peter Haule, WFM, Zanzibar)
**************************
Na Benny Mwaipaja, Zanzibar
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kukuza uchumi wa Zanzibar kupitia sekta za uchumi wa blue pamoja na utalii.
Mheshimiwa Masauni ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kikazi kwenye Tawi la Benki Kuu ya Tanzania lililoko kisiwani Unguja-Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Alisema kuwa Zanzibar inategemea uchumi wa blue ikiwemo masuala ya uvuvi pamoja na sekta ya utalii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake hivyo utafiti katika Nyanja hizo utasaidia kubaini njia bora za kuharakisha ukuaji wa uchumi wake kupitia Sekta hizo muhimu.
“Mazingira ya Uchumi wa Zanzibar ni tofauti na mazingira ya uchumi wa Bara, kuna maeneo ambayo katika uchumi wa Zanzibar yamepewa kipaumbele likiwemo suala la uchumi wa blue, na utalii, hivyo kuna kila sababu Benki Kuu ya Tanzania kufanya tafiti katika maeneo hayo ili kuishauri vema Serikali”, alieleza Mhandisi Masauni.
Kwa upande wake Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aneyesimamia uthabiti wa sekta ya fedha pamoja na kusimamia Tawi la Benki Kuu-Zanzibar Dkt. Bernard Kibesse amemhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa MHandisi Hamad Yussuf Masauni kwamba maelekezo aliyoyatoa yatatekelezwa.
Alisema kuwa Benki hiyo tayari imeanza mchakato wa kufanya tafiti mbalimbali zitakazo saidia kukukuza na kuimarisha uchumi wa Zanzibar pamoja na kutekeleza sera za fedha kwa manufaa ya nchi hiyo na Taifa kwa ujumla.
“Tumesikiliza maagizo yako hasa ya kufanya tafiti kuhusu hali ya uchumi wa Zanzibar kwa kujikita zaidi katika uchumi wa Blue na utalii maeneo ambayo ndiyo nguzo kuu za uchumi wa Zanzibar”, alieleza Dkt. Kibesse.
Naye Mkurugenzi wa BoT Tawi la Zanzibar Dkt. Camillius Kombe alieleza kuwa Sera imara za fedga zimeiwezesha Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuwa na uchumi imara pamoja utulivu wa mfumuko wa Bei ambao hivi sasa hauzidi asilimia moja.
Alisema kuwa kumekuwepo na utulivu wa bei visiwani Zanzibar kwa muda mrefu, ambao unatokana na Sera za Fedha kuwa na ufanisi kwa upande wa Zanzibar na imetokana na BoT Zanzibar kutoa hali halisi na mikakati ya kukuza uchumi na kuipeleka kwa watoa maamuzi