Home Mchanganyiko MWENGE UMEZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YA SHILINGI BILIONI 1.4 WILAYANI KALIUA

MWENGE UMEZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YA SHILINGI BILIONI 1.4 WILAYANI KALIUA

0

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (kushoto) akipokea leo Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon sengati(kulia) tayari kwa kuanza mbio zake katika Wilaya saba za Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru leo baada ya kuupokea kutoka Mkoani Shinyanga tayari kwa kuanza mbio zake katika Wilaya saba za Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Chacha (kushoto) Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuanza mbio zake katika Wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamepanda kwenye miti leo katika Kijiji cha Uyowa wilayani Kaliua kwa ajili ya kutaka kushuhudia Mwenge wa Uhuru ulianza mbio zake Mkoani Tabora

Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi (wa pili kutoka kushoto) akikagua leo majengo ya Kituo cha afya cha Uyowa kilichopo wilayani Kaliua kabla za kuzindua.

Picha na Tiganya Vincent

*****************************

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA

MWENGE wa Uhuru umezindua miradi sita ya maendeleo yenye jumla ya shilingi bilioni 1.4 wilayani Kaliua.

Kati ya fedha hizo Serikali kuu imetoa shilingi bilioni 1.3, Halmashauri imechangi milioni 107.9, michango ya wananchi milioni 19 na michango ya sekta binafsi imechangia milioni 4.6.

Uzinduzi huo umefanywa leo na Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kaliua.

Katika mradi wa kwanza mwenge wa uhuru umetoa mikopo ya pikipiki yenye thamani ya shilingi bilioni 76.2 kwa vikundi vya vijana Kata ya Sasu, Nhwande na Usenye.

Luteni Josephine aliwataka vijina ambao hawana Leseni kutoendesha Pikipiki hizo kabla ya kupata mafunzo yatakayowasaidia kujikinga na ajali na kujiepusha kuwasababishi watu wengine ajali.

Kiongozi alizindua mradi wa maji ya bomba Mji w Kaliua ambao umegharimu shilingi milioni 571.6.

Akizindua mradi huo aliwataka Watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) kuhakikisha wanawashirikisha wananchi toka hatua za awali za utekelezaji wa miradi ili iweze kuwa endelevu na wao sehemu ya mradi husika.

Akiweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Kituo cha Afya Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kumazilia haraka majengo yaliyobaki ya Kituo cha Afya cha Uyowa ambacho yanatarajiwa kugharimu cha Afya Uyowa utakaogharimu shilingi milioni 648.6.

Alisema kwa kuwa fedha zipo hakuna haja ya kuchewesha ujenzi wa Kituo hicho ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.

Luteni Josephine alizindua Mnara wa Kampuni ya Simu ya Tanzania(TTCL) katika Kijiji cha Ulindwanoni ambao umegharimu shilingi milioni 173 na ukaguzi wa mfumo wa CCTV Kamera katika Stendi mpya ya mabasi Kaliua.

Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuanzisha Kamera ya Usalama katika Kituo cha Mabasi ambayo imewasaidia kudhibiti upotevu wa mapato na kutekeleza kwa Vitendo ujumbe wa Mwenge wa Mwaka huu ambao ni Tehama ni Msingi wa Taifa endelevu ;itumie kwa usalama na uwajibikaji.