Home Biashara WMA YAJIPANGA KUHAKIKISHA VIPIMO VYA KUPIMA MADINI VINAKUWA SAHIHI NA KUWEZA KUKUZA...

WMA YAJIPANGA KUHAKIKISHA VIPIMO VYA KUPIMA MADINI VINAKUWA SAHIHI NA KUWEZA KUKUZA SOKO LA MADINI NCHINI

0

*********************

Katika kuhakikisha nchi inakua Kiuchumi kupitia sekta ya Madini, Wakala wa Vipimo (WMA) wamekuwa wakihakikisha mizani ambazo zinatumika kwaajili ya kupima madini ni sahihi na inayota matokeo yanayokusudiwa.

Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Wakala wa Vipimo(WMA) Mkoa wa Geita Bw.Moses Ntungi amesema Vipimo vyetu lazima vitambulike Kimataifa kwamaana kipimo kilichopimwa hapa nchini kinaendana na vipimo vya kimataifa, kwahiyo tunauwezo wa kuuza madini kwa lugha inayoeleweka ya vipimo. 

“Madini yatakapopimwa hapa Tanzania yakaenda katika mataifa mengine itakuwa ni kilo hizohizo kwahiyo tumekuwa tukijitahidi kuhakikisha kwanza toka dhahabu ama madini mengine yanapokuwa yanazalishwa yanapitia katika vipimo ambavyo ni sahihi mpaka itakapokuwa tayari kwaajili ya export inatumia vipimo ambavyo ni sahihi”. Amesema Bw.Ntungi.

Amesema ili uweze kupata faida kwenye biashara yoyote ile vipimo ni muhimu, kwamaana ili uweze kupiga hesabu zako vizuri na kuthaminisha bidhaa zako ni lazima iwe na vipimo kwahiyo wao kama Wakala wa Vipimo kazi yako ni kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika maeneo ya madini ni vipimo vilivyohakikiwa na wakala