Home Biashara MAKAMU WA PILI WA RAIS MHE.HEMED ABDULLAH KUFUNGA MAONESHO YA 45...

MAKAMU WA PILI WA RAIS MHE.HEMED ABDULLAH KUFUNGA MAONESHO YA 45 YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA)

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Hemed Abdullah anatarajiwa kufunga Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya mwalimu Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigae amesema kuwa siku ya kufuna Maonesho hayo mgeni Rasmi atatoa tuzo kwa washindi wa zoezi la ukaguzi wa banda bora.

Aidha ametoa wito kwa watembeleaji ambao hawajapata nafasi ya kufika katika uwanja wa Maonesho kutumia siku hizi chache zilizobaki ili waweze kufika na kujionea bidhaa na huduma mbalimbali zinatolewa na makampuni, Wizara na Taasisi mbalimbali.

Amesema utekelezaji wa miongozo na tahadharizote za kujikinga na ugonjwa wa UVICO-19 zinatolewa na Wizara ya Afya zinatekelezwa ipasavyo kwa kushirikiana na kamati maalumu ya kitaifa ya masuala ya afya wakati wote wa maonesho hayo.

“Kupitia miongozo hiyo  tumeweza kupunguza masongamano katika milango ya kuingia kwa kuhamasisha watembeleaji kukata tiketi kwa njia ya mtandao, kunawa mikono  kwa maji tiririka na sabuni, kuweka vitakasa mikono  maeneo mbalimbali ya uwanja na uvaaji wa barakoa”. Amesema Mhe. kigae.