Home Siasa CHONGOLO AENDELEA NA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA NA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI...

CHONGOLO AENDELEA NA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA NA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI WILAYANI KYELA MKOA WA MBEYA

0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo, leo tarehe 12 Julai, 2021  ameendelea na ziara yake ya kuimarisha Chama Mashinani katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya ambapo amefanya vikao katika shina namba 10 tawi la Ipinda na Shina namba 01 Tawi la Fubu.
Aidha, katika kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ametembelea maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mwambusye kata ya Ikama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akifurahia jambo wakati akizungumza katika mkutano wa wanachama wa shina namba 1 katika kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akizungumza katika mkutano wa wanachama wa shina namba 1 katika kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akitoa Vitendea kazi kwa Balozi wa  shina namba 1 katika kijiji cha mwambise kata ya Fubu Ndg  Seth S Mwambandile, leo 12, julai 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akikagua kikundi cha ngoma alipowasili katika ukaguzi  wa utekelezaji wa Ilani ya CCM  2020-2025 wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM  katika ukaguzi  wa utekelezaji wa Ilani ya CCM  2020-2025 waujenzi wa Zahanati ya kijiji cha mwambise kata ya Fubu, leo 12, julai 2021.

 Mwanachama Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi Sambina Igende akifurahi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM katika kikao Cha Wanachama wa Shina No 1 kata ya Ikama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (aliyevaa Barakoa)  akikagua  Ujenzi wa  Mabweni ya Wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Kafundo katika kata ya Ipinda , leo 12, julai 2021.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndg Jacob Mwakasole pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyela Ndg Patrick Mwampele  akitoka kugagua  Ujenzi wa  Mabweni ya Wanafunzi wa kike ( pichani nyuma) katika Shule ya Sekondari Kafundo katika kata ya Ipinda , leo 12, julai 2021. (Picha Zote na CCM Makao Makuu)