Home Burudani MISS TANGA 2021 KUMEKUCHA FOMU ZA USHIRIKI KUANZA KUTOLEWA AGOSTI 1 MWAKA...

MISS TANGA 2021 KUMEKUCHA FOMU ZA USHIRIKI KUANZA KUTOLEWA AGOSTI 1 MWAKA HUU

0

Muandaaji
wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double
Touch Entertainment Chuchu
Hans akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini
Tanga kuhusu kushoto ni Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati
wa mashindano kulia ni Mwalimu ambaye
atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji

Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu
Double Touch Entertainment Chuchu
Hans akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini
Tanga kuhusu kushoto ni Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati
wa mashindano kulia ni Mwalimu ambaye
atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji

Wilson
Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati
wa mashindano akizungumza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni
Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021  kupitia Kampuni yake ya Chuchu
Double Touch Entertainment Chuchu
Hans akifuatiwa na Mwalimu ambaye
atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji

Mwalimu
ambaye
atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji akizungumza jambo wakati wa
mkutano huo kushoto ni Muandaaji wa Shindano la Miss Tanga 2021 
kupitia Kampuni yake ya Chuchu
Double Touch Entertainment Chuchu
Hans akifuatiwa na Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati
wa mashindano hayo

Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakichukua matukio kwenye mkutano huo

SHINDANO la kumsaka Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga
2021) limeiva baada ya kamati inayoandaa mashindano hayo kutangaza
kwamba Agosti 1 mwaka huu fomu za usaili zitaanza kutolewa kwa
washiriki.

Hayo yalibainishwa leo na Muandaaji wa Mashindano
hayo kupitia Kampuni yake ya Chuchu Double Touch Entertainment Chuchu
Hans wakati mkutano wake na wandishi wa habari uliofanyika mjini Tanga
ambapo alisema maandalizi yote yamekamilika.

Alisema kwamba
msimu huu wamejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na mvuta
na ushindani huku akieleza kwamba yatawahusisha zaidi wakazi wa Tanga.

“Hivyo kupitia mkutano huu niwaalike wakazi wa Mkoa huu na wilaya zake
na vitongoji kuchangamkia fursa ya kushiriki mashindano haya kwa sababu
mashindano ya Urembo ni heshima na kazi”Alisema

Akizungumza
namna walivyojipanga kuyafanyia kuwa ya kipekee tofauti na miaka ya
nyumba alisema waliandaa Miss Tanga 2019kwa mara ya mwisho kabla ya
kuingia Covid 19 na walikua bora katika uandaaji hivyo wataendelea
kuboresha zaidi katika shindano la mwaka huu

“Ndugu zangu
mjitokeze kwani urembo ni heshima na kama mnavyoona warembo wanapata
nafasi mbalimbali za uongozi lakini pia ni ajira hivyo washiriki
wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa “Alisema

Kwa upande wake
Wilson Untouchable ambaye ni mmoja wa wanakamati wa mashindano
hayo alisema washiriki wote wanan afasi ya kushinda na wakipata nafasi
ya kuingia kwenye mchujo tayari ni mshindi kwa kuwa wote zawadi
watapata.

Untouchable alisema ukiachana na washindi
watatu,waliobaki watapata fursa za nafasi mbalimbali kupitia wadhamini
kwani kuna mdhamini anaweza kumuona mshiriki akawa Balozi wa bidhaa
Fulani katika kampuni yake.

Naye kwa upande wake Mwalimu ambaye
atakuwa akiwanoa walimbwende hao Pili Miraji aliwataka mabinti wa mkoa
huo kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye mashindano hayo .

Alisema
kwa kuwa hakuna mshiriki anayepangwa kwa ajili ya kuwa Mshindi amesema
hilo kwao halipo na halitatokea katika mkoa wa Tanga.

“Ndugu
zangu msiwe na wasiwe wala woga kuhusu mchakato wa Mshindi upo wazina
hata Miss Tanzania imebadilika kwa kuwa waandaaji wengi wamekuwa
washiriki wa Mashindano ya Ma-Miss kwa miaka ya nyuma,hivyo ubora wa
Mshindi ni kutokana na vigezo na kujiandaa kwake kuwaMshindi”alisema
Pili.

Pia wameomba wadhamini wajitokeze kwa wingi ili mashindano yaweze kunoga na washiriki waweze kufaidika.