Home Mchanganyiko ZIARA YA RAIS DKT.MWINYI MKOA WA MJINI MAGHARIBI

ZIARA YA RAIS DKT.MWINYI MKOA WA MJINI MAGHARIBI

0

Ameir Simai Hassan mkaazi wa Mtofaani akitoa ushauri kwa watendaji wa serikali kuwajibika ili kumpunguzia  majukumu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuwaombea wananchi wake mahitaji maalumu ikiwemo maji na barabara .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na wananchi wa shehia ya Welezo na shehia jirani kuhusu changamoto zinazowakabili ikiwemo maji na barabara za ndani katika ziara yake ya kukagua shughuli za kimaendeleo ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi.

Fatma Said Mohd mkaazi wa Uholanzi akizungumzia changamoto ya barabara za ndani wakati wa ziara ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Baadhi ya visima vya asili vilivyopo katika shehia ya Welezo Wilaya ya Magharibi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mradi wa uhaulishaji na uimarishaji huduma za maji wa EXIM Bank ukiendelea katika shehia ya Dole Wilaya ya Magharib “A” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa ZAWA Dkt. Hafsa kuhusu kisima cha maji kilichopo Bumbwi Sudi kinachosambaza maji shehia za Mjini wakati wa ziara yake ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi.

PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR.