Home Mchanganyiko RC MTAKA AWATAKA VIONGOZI KUTOKUWA KIKWAZO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO

RC MTAKA AWATAKA VIONGOZI KUTOKUWA KIKWAZO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya Viongozi wa Mkoa huo na Wafanyabiashara wadogo wadogo  jijini Dodoma.Mmoja wa Wafanyabiashara wadogo wa Jiji la Dodoma aliyetambulika kwa jina la Dangote akitoa maoni yake kwenye mkutano wa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka  jijini Dodoma.
Wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa, Anthony Mtaka katika mkutano wa pamoja uliolenga kutatua changamoto za wafanyabiashara hao jijini Dodoma.

……………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewaagiza viongozi wa serikali kuanzia mamlaka za chini kutokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara ndogo ndogo jijini humo badala yake wawe sehemu ya kuwawezesha kukua kibiashara na kufikia malengo yao.

Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na  wafanyabiashara ndogo ndogo jijini humo ambapo pamoja na mambo mengine, amesikiliza kero na changamoto zinazowakabili katika biashara zao.

“Lakini pia na ninyi wafanyabiashara nawasihi kuzingatia sheria na kanuni za kufanya biashara ili msilete athari kwa wananchi wengine wakati wa kutimiza majukumu yenu,” amesema.

Katika mkutano huo pia wafanyabiashara wadogo waliiomba serikali iwapange vizuri katika maeneo hayo na kurasimisha baadhi ya maeneo ili wasipate bugudha kutoka kwa askari na migambo wa jiji.

Mkutano huo uliowakutanisha Wafanyabiashara wadogo kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma, ulihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dk. Fatma Mganga, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma,Wakuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.