KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shaibu Akwilombe, akizungumza na Baraza la Wazee la Mkoa huo, wakati wa hafla ya kujitambulisha, jana. Kuroka kushoto ni Katibu wa baraza hilo, Mohammed Mtulia, Mwenyekiti wa Baraza mkoani humo, Hemmed Mkali na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba.

**************************

Na CHRISTOPHER LISSA

 BARAZA la Wazee la Mkoa wa Dar es Salaam, limembariki Katibu wa Chama Cha  Mapinduzi (CCM) wa   mkoa huo, Shaibu Akwilombe na kuahidi  kumpa ushirikiano wa kutosha.

Hayo yamesemwa wakati wa hafla  ya Akwilombe  kujitambulisha  kwa wazee hao , jijini Dar es Salaam, ambapo  baraza lilimhakikishia ushirikiano katika kukijenga chama.

Akizungumza  kwa niaba ya wazee wa mkoa huo, Mwenyekiti wa  baraza hilo,  Mohammed Mkali, alisema  hata kabla ya Akwilombe kujitambulisha, wazee  mkoani humo wameridhishwa na kasi ya utendaji wake aliyoanza nayo.

“Tunaomba uendelee na kasi hiyo. Wazee tuko pamoja na wewe katika kutekeleza Ilani ya CCM na kumsaidia Rais  Samia Suluhu Hassan katika  kutekeleza Ilani hiyo,”alisema  Mkali.

Kwa upande wake Akwilombe, aliahidi  kushirikiana na wazee hao na kwamba Baraka zao zinamfanya kupata  faraja ya kuendeleza mapambano katika kukipigania Chama.