Home Mchanganyiko MILIONI KUMI NA MOJA NA LAKI TANO ZATOLEWA KUSAIDIA VIKUNDI SONGEA MJINI

MILIONI KUMI NA MOJA NA LAKI TANO ZATOLEWA KUSAIDIA VIKUNDI SONGEA MJINI

0

NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MBUNGE wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro  Waziri wa Maliasili na Utalii ametoa fedha kiasi cha shilingi  Milioni kumi na moja na laki tano kwa vikundi 17 ndani ya Halmashauri ya Songea kwa lengo la kuinua vikundi vya wajasiriamali ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika  wanavikundi hao.

Zoezi hilo limefanyika Manispaa ya Songea na kusimamiwa na  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano  ambaye alikuwa akimwakilisha  Mbunge  wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Maliasili na Utalii.

Mbano alisema Manispaa ya Songea ina  jumla ya vikundi 21 vya wajasiliamali   kati ya hivyo vikundi 17 vimewezeshwa kupata mkopo, na vikundi 4 havikukidhi vigezo vinavyokubalika.

Amewataka wajasiriamali waliopokea fedha hizo kuhakikisha wanazitumia matumizi sahihi ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo na kukamilisha miradi  iliyoanza kufanyika katika vikundi vyao  na  kuwasaidia kujikwamua kiuchumi wao binafsi na kuleta maendeleo kwenye jamii inayowazunguka. ‘Mbano alisisitiza’.

Naye Mratibu wa vikundi ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Alela Yazidu Kapinga amesema jumla  ya vikundi 17  vyenye jumla ya wanachama 417 wamepokea fedha kutoka kwa Mbunge wa Songea Mjini yenye jumla ya  thamani ya shilingi   milioni kumi na moja na laki tano  kwa wajasiliamali  wanaojishughulisha na  miradi mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa bidhaa za  sabuni, ufugaji wa kuku na kilimo.

Kwa nyakati tofauti wakitoa shukrani za dhati  wajasiriamali hao  “walisema wanashukuru kwa msaada uliotolewa na Mbunge  Dkt. Damas Ndumbaro  ambapo wameahidi  kuendeleza miradi ya vikundi  kwa kuwezeshana pamoja na kubuni miradi mingine  mipya yenye tija kwa ajili ya ustawi wa  vikundi vyao.”

Fedha hizo hazijatolewa kama mkopo  na hazina riba, kwa lengo mahususi  la kuwainua wajasiliamali wadogo wadogo  waishio  Songea Mjini.