Home Mchanganyiko WATUMISHI TUMIENI UTAALAMU WENU KUONDOA KERO ZA WANANCHI

WATUMISHI TUMIENI UTAALAMU WENU KUONDOA KERO ZA WANANCHI

0

Mkuu wa wilaya anayemaliza Muda wake January Lugangira akimkabidhi
Ofisi Mkuu wa wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro mapema leo wilayani humo
picha zote na Ahmed Mahmoud Lushoto

Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Lushoto
wakiwa kwenye makabidhiano ya Ofisi mapema leo wilayani Lushoto kama
walivyokutwa na Kamera ya Matukio picha zote na Ahmed Mahmoud Lushoto.

***********************

Na Ahmed Mahmoud Lushoto

Mkuu wa wilaya ya Lushoto kalisti Lazaro amewataka watumishi wa umma
wilayani humo kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kwa wakati
ikiwemo sekta ya elimu kwa shule za awali kufanya vibaya pamoja na
waalimu kuhama vituo vya kazi na kukimbilia maeneo ya mjini.

 Ameyasema hayo Mara baada ya Kukabidhiwa Ofisi na Mtangulizi wake
January lugangika Mapema Leo mjini Lushoto alisema amepokea changamoto
zote alizo somewa na kuahidi kwamba atashirikiana na watendaji wa
ngazi za Wilaya zote tatu pamoja na wataalamu wake wa Wilaya
kuakikisha wanatatua changamoto zote katika Wilaya yake.

Alisema kuwa changamoto ya uwepo wa wimbi la walimu kuhama
halikubaliki hivyo amajipanga kuhakikisha anatatua kero hiyo kwa
kushirikiana na watendaji wengine ndani ya serikali kuona namna nzuri
ya waalimu kuona eneo hilo ni sehemu ya Tanzania na sio sehemu ya
kupatia ajira.

Lazaro ametumia muda huo pia kumshukuru Mh rais Samia Suluhu Hassan
kwa uteuzi huo kuwa mkuu wa Wilaya na kuahidi kufanya kazi ya
kumsaidia katika utendaji kwa kufuata ilani ya chama cha mapinduzi Ccm
kuwaletea maendeleo wananchi wa Lushoto kwa haraka zaidi.

Amesema alishakua mtendaji kwa nafasi ya Meya katika jiji la Arusha
kutatua migogoro ya Ardhi changamoto ya sekta ya elimu atatumia uzoefu
wake huo huhakikisha wilaya hiyo inapiga hatua kwa kushirikiana na
wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati.

Awali akiongea Mara baada ya kukabidhi Ofisi January Lugangira Amesema
kwa muda wote aliyetumikia Wilaya hiyo takribani miaka sita kumekuwepo
na changamoto ya shule za awali kufanya vibaya katika matokeo ya
mitihani na wanafunzi kutoroka masomo jambo linalo rudisha nyuma
taaluma ya elimu katika Wilaya ya lushoto Mkoani Tanga

 Amemuomba mkuu Huyo mpya wa Wilaya kalisti Lazaro kwa kushirikiana na
viongozi wa elimu katika Wilaya hiyo kuboresha sekta ya elimu pamoja
na kupiga vita suala la waalimu kuhama vituo vya kazi ameeleza pia
changamoto ya afya ikikabiliwa na madereva wa kuendesha magari ya
wagonjwa kukaa mbali na vituo vya kazi na kusababisha kunapotokea
mgonjwa kushindwa kumuhudumia kwa muda unaohitajika

”Unakuta Dereva anaacha gari katika kituo cha kazi yeye anakwenda
kuishi mjini tatizo linapotokea kijijini inakuwa ni vigumu kumpatia
msaada wa haraka na muda mwingi kusababisha mgonjwa kupoteza maisha au
kucheleweshewa matibabu hivyo Mh Mkuu wa Wilaya naomba ulisimamie hilo
pamoja na upungufu wa madawa katika vituo vya afya alisema mkuu wa
Wilaya aliye maliza muda wake January  lugangika ”

Naye Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya lushoto Mkoani Tanga Rashid Hassan
Amemshukuru Mh Rais Samoa Suluhu Assam kwa uteuzi wa mkuu wa Wilaya
mpya ya lushoto na kusema kwamba wapo tayari kumpa ushirikiano
kumshauri na kutumikia wananchi katika kutatua matatizo ususani kufika
katika makazi yao kusikiliza changamoto mbali mbali zinazo wakabili .

Pia amesema kwamba chama chamapinduzi Ccm katika Wilaya zake
inamajimbo matatu ya uchaguzi ikiwa inashikiliwa na Ccm na Ccm pamoja
na madiwani wote kutokea Ccm pamoja na na mwenyeviti wa vitongoji
vijiji hivyo mkuu wa Wilaya kalisti Lazaro atapata ushirikiano katika
kutimiza majukumu yake.