Home Siasa UWT DAR TUTANYAKUA MADARAKA UCHAGUZI WA CCM

UWT DAR TUTANYAKUA MADARAKA UCHAGUZI WA CCM

0

***********************

NA MWANDISHI WETU

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT), umewataka wanawake kujitokeza kwa wingi, kugombea nafasi za uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa ndani wa Chama unaotarajiwa kufanyika Mwakani.
Hatua hiyo ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuteleza ajenda ya asilimia 50 kwa 50 katika kwenye ngazi za maamuzi kati ya wanaume na wanawake.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Florance Masunga aliyasema hayo wakati akizungumza na wanachama na viongozi wa UWT wa Jimbo la Kawe.

Florance, alisema ni lazima wanawake kushika nafasi za maamuzi ambapo katika uchaguzi ujao wanawake wajitokeze kwa wingi.
Florance alieleza, Rais Samia amekuwa akitekeleza ajenda ya 50 kwa 50 kwa vitendo ambapo hata kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya awamu hii ameteua wanawake zaidi ya 40.

Naye Katibu wa UWT wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule, alisema kwenye uchaguzi huo wa ndani ya Chama, wanawake wata teka mamlaka.
“Sisi ndiyo roho ya Chama na jumuia zake. Awamu hii amkeni tunyakue mamlaka. Rais wetu ni mwanamke hivyo huu ndiyo wakati wetu wanawake kusimama na kuteka mamlaka,”alieleza Grace.