Balozi mstaafu Njoolay akifurahia jambo na Mratibu wa mpango huo, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe. |
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Masyenene akiishukuru Kamati ya Uongozi inayomaliza muda wake kwa ushirikiano mkubwa walioufanya wakati wa uongozi wao. |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MKURABITA, Glory Mbilimonya akiongoza hafla hiyo. |
Sasa ni wakati wa kuserebuka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, anayemaliza muda wake, Balozi Njoolay (aliyekaa katikati) akiwa na baadhi wajumbe wa pamoja na baadhi ya watumishi wa MKURABITA. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA), anayemaliza muda wake, Balozi Daniel Ole Njoolay ameishukuru Menejimenti na watumishi wa mpango huo kwa kuwa
wasikivu kutekeleza maagizo waliyokuwa wanawapatia ndani ya miaka mitatu
ya uongozi wao.
Balozi Njoolay, ameyasema hayo wakati wa hafla
fupi ya MKURABITA kuiaga kamati hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Mpango huo
katika Hoteli ya Collina, jijini Dodoma.
Njoolay amesema kuwa
usikivu na uchapakazi wao ndiyo umewezesha MKURABITA kuwa na mafanikio
makubwa na kuwataka waendelee na moyo huo na kuisapoti kamati nyingine
itakayokuja baada ya wao kuondoka.
“Kwa niaba ya wajumbe wenzangu
napenda nichukue nafasi hii kuishukuru menejimenti, mmekuwa wasikivu
kwa yale maelekezo tuliyokuwa tunawapatia asanteni sana. Pili
niwashukuru wajumbe wenzangu wa kamati, sijapata shida kama kiongozi
walinipa ushirikiano mzuri, tunaongea vizuri, hakuna kufokeana
tunaelewana na kufikia makubaliano.” amesema Njoolay.
Aidha, ili
kuboresha utendaji na mahusiano kazini, Balozi Njoolay ameutaka uongozi
wa MKURABITA kuanzisha Family Day itakayowajumuisha viongozi, watumishi
na familia zao ambapo watacheza kwa pamoja na kufahamiana zaidi.
Amesema
kuwa wakifanya hivyo utendaji kazini utaongezeka bila wao kujua, lakini
pia mchanganyiko huo utaongeza uhusiano miongoni mwao na kuwa wamoja.
Ametoa
mfano kuwa akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo,
alianzisha Family Day baada ya kuwakuta wafanyakazi hali yao ikiwa si
nzuri, kitendo ambacho kiliamsha ari ya ufanyakazi na kujenga uhusiano
mzuri miongoni mwao na familia zao kwa ujumla.
Pia, akiwa Balozi
wa Tanzania nchini Nigeria, baada ya kukuta hali ya utengano kati ya
watumishi wa kawaida na maofisa wa ubalozi, aliamua kuanzisha Family
Day, jambo ambalo lilisaidia sana kujenga umoja na utendaji kazi
ukaongezeka. Alipowatangazia kuwa anarejea nchini watumishi ambao
asilimia kubwa walikuwa ni wanigeria walilia machozi na kusababisha hata
yeye kulia.
“Mchango wenu kwa muda wa miaka mitatu mliokuwa nasi
ni mkubwa sana, si kwa kusifia tu, bali huo ndiyo ukweli, kuna vitu
mmefanya vinavyotufanya sisi tufuate, Uongozi wa kutufanya
tuwasikilize, tusikie hamu ya kutekeleza uliyoyasema na bodi yako,
tunawashukuru sana,” alianza kwa kusema hayo Mratibu wa MKURABITA,CPA, Dkt Seraphia Mgembe.
CPA,Dkt. Mgembe amesema kuwa moja ya
mambo aliyomuachia Njoolay atakayokumbuka daima na kuendelea nayo katika
uongozi wake ni kwamba ukiwa kiongozi kabla ya kumfanyia jambo mtu
mwingine au mfanyakazi wako “Lionje kwanza ukikuta chungu usimfanyie
mfanyakazi, na ukionja ukikuta tamu basi mfanyie. kwa kipindi chote cha
ufanyakazi wako Njoolay umekuwa ukifanya hivyo,” alisema Dkt. Mgembe.
“Kwa
kipindi cha uongozi wenu utekelezaji wa maelekezo yenu umeleta chanya
MKURABITA, tunawashukuru sana kwa uongozi wenu mwema, tunaamini huko
mwendako mtakuwa mabalozi muisemee vizuri MKURABITA ili urasimishaji
usonge mbele,” hayo ni maneno ya Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa MKURABITA, Jane Lyimo.
Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Masyenene alisema kuwa uwepo wa kamati hiyo yenye watalaamu wengi, wamejifunza mengi na kuwafanya iwe rahisi kutekeleza malengo yao, na kwamba wataendelea kufanya mawasiliano nao ili waendelee kuchota utalaamu huo kwa lengo la kuendelea kuboresha ajenda ya urasimishaji nchini.
Kamati hiyo ambayo ilianza kazi 2018/2018 imeongoza kwa muda wa miaka mitatu hadi 2021. Kabla hapo alianza John Chiligati na kufuatiwa na aliyekuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Kamati ya Uongozi inayomaliza muda wake ni;