Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI SILINDE ATOA MIEZI 2 KWA TARURA KUJENGA DARAJA,TABATA KIMANGA

NAIBU WAZIRI SILINDE ATOA MIEZI 2 KWA TARURA KUJENGA DARAJA,TABATA KIMANGA

0

…………………………………………………………………………..

Mwandishi wetu, Dar es salaam

Naibu waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. David Silinde, ameigiza halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wakala wa Barabara za mjini na Vijijini TARURA Mkoa wa Dar es salaam, wafanye taasmini ya haraka na kisha kuanza ujenzi wa daraja katika barabara ya mtaa wa sokoine kimanga.

Naibu Waziri Silinde amefikia adhma hiyo wakati wa ziara katika jimbo la Segerea kukagua ubovu wa barabara za ndani ya jiji la Dar es salaam na kubaini kutotumika kwa barabara hiyo kutokana na daraja ambalo hutumika kuharibiwa na mvua na kuhatarisha maisha ya wananchi wa maeneo hayo.

Silinde ametoa miezi miwili daraja lianze kujengwa na kuahidi kurejea katika eneo hilo kwaajili ya kukagua kujionea utekelezaji wake.

“Huu sio muda wa kubishana bali fanyeni tathimini ya gharama za ujenzi na ujenzi uanze mara moja iwe wakati wa mvua au jua kwakuwa umuhimu wa daraja hili kwa wananchi ni muhimu sana” amesema Silinde.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamol, amemuomba Naibu waziri Silinde kupatiwa barabara katika jimbo lake, kwakuwa wao wamesahuliwa kwa muda mrefu na barabara nyingi hazipitiki vizuri, hivyo wakaomba kukumbukwa katika bajeti ijayo kupelekewa barabara za lami kwenye mitaa ili kuwasaidia wananchi wa jimbo la segerea.

Akiongea kwa niaba ya wanananchi wenzake mkaazi wa mtaa Sokoine, Twaha Saidi amemuelezea Naibu waziri kwamba, kwa sasa barabara husika ni kiunganishi kwao, lakini imegeuka kuwa eneo hatarishi, kwakuwa hadi sasa wamefanikiwa kuokoa watoto wawili ambao walibebwa na maji wakati wa mvua, wakiwa wanajaribu kuvuka katika mto unaopita katika Barabara hiyo.