Home Mchanganyiko MGOGORO WA ARDHI BAINA YA JESHI NA WANANCHI WATAFUTIWA SULUHU

MGOGORO WA ARDHI BAINA YA JESHI NA WANANCHI WATAFUTIWA SULUHU

0

*****************

Na Bahati Habibu Maelezo  19/06/2021    Maelezo Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeunda kamati ya kufuatilia tatizo la mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na Kambi ya Jeshi la Wananchi katika kijiji cha Ubago kilichopo Wilaya ya Kati Unguja.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa  Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi  amesema tayari imeshaundwa kamati ya kufuatilia upimaji wa maeneo yote yenye migogoro ya ardhi katika Mkoa huo kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.

Amesema ofisi ya Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi imeanza kuyakagua maeneo hayo ili kuangalia mipaka kwa ajili ya hatua ya upimaji.

Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa mgogoro wa ardhi uliomo katika mkoa huo unasababisha migongano baina ya wananchi na Jeshi la Wananchi katika kambi ya Ubago na baadhi ya maeneo ya vjiji vya jirani na kupelekea uhasama kwa jamii

Bwana Hadidi amewataka wananchi kuwa wastahamilivu wakati Serikali inalishughulikia tatizo hizo  na kulitafutia ufumbuzi ili jamii ipate kuishi kwa amani na mashirikiano mazuri na serikali.

“Ndugu zangu wananchi wa Ubago tutulie na tuamini Serikali inayoongozwa na Dkt Mwinyi ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kwa kuwapa huduma bora ikiwemo kuwatatulia changamoto zinazowakabili ili waishi kwa amani”, alieleza Mkuu wa Mkoa huyo.

Hata hivyo amewasisitiza wakaazi wa maeneo yenye migogoro kutoa ushirikiano na watendaji wa wizara ya ardhi wakati watakapopita katika meneo yao kutoa maelezo ya kina ili kuweza kufankiisha zoezi hilo na kufikia lengo lilikusudiwa na  kuondokana na  changamoto hiyo.

Katika utekelezaji wa zoezi la upimaji wa maeneo yenye migogoro ya ardhi Mkuu huyo wa Mkoa amemtaka sheha wa shehia ya Ubago kuunda kamati ya watu kumi na mbili (12) watakaowakilisha wananchi kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Mapema Mkuu wa Wilaya Kati Bi Marina Joel Thomas amewataka wananchi wa Ubago kuzitumia ofisi za Wilaya kuyafikisha malalamiko kwa lengo  la kupatiwa ufumbuzi na kuchukuliwa hatua husika .

Nao Viongozi wa Jimbo la Tunguu wameahidi kutoa mashirikiano kwa Serekali ili kuona migogoro iliomo ndani ya jimbo hilo  inapatiwa suluhu ya kudumu.

Nao wananchi wakijiji cha Ubago wameiomba Serikali kuupatia ufumbuzi wa haraka mgogoro huo pamoja na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kambi ya Jeshi hilo ili kuwaruhusu kufanya shughuli zao za kilimo na uchimbaji kwa kujipatia kipato na kujikimu kimaisha.

Aidha wananchi hao wameeleza kuwa wapo tayari kuipisha Kambi hiyo ya Jesho kwa makubaliano ya kupatiwa maeneo mengine ya makaazi na sehemu za kujikimu kimaisha kwa ajili ya kilimo na shughuli nyengine