Home Mchanganyiko KAIMU RC AAGIZA WALIOHISABABISHIA HOJA NZEGA WACHUKULIWE HATUA

KAIMU RC AAGIZA WALIOHISABABISHIA HOJA NZEGA WACHUKULIWE HATUA

0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP ) Advera Bulimba (kushoto ) akibadilishana mawazo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Seleman Sikiete (katikati) mara baada yta kukamilika kwa  Baraza Maalum la Madiwani la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP ) Advera Bulimba akitoa maelekezo kwa Menejinenti ya  Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakati mkutano wa  Baraza Maalum la Madiwani la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa ufafanuzi jana wakati wa   Baraza Maalum la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nzega  kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
******************************
NA TIGANYA VINCENT
 

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega limeagizwa  kuhakikisha linawachukulia hatua watumishi wote waliosababisha hoja zilizotokana na uzembe ikiwemo upotevu , mapato, manunuzi yasiyofuata taratibu  pamoja na usimamizi usioridhisha wa miradi ya Maendeleo.

 

Kauli hiyo imetolewa  na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP ) Advera Bulimba wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega la kupitia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

 

 Alisema hatua hiyo itasaidia kuepuka kurudiwa kwa makosa ambayo yameisababisha Halmsahauri hiyo kupata Hati yenye mashaka.

Aidha Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa ameigaiza Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kuhakikisha inafuatilia na kurejesha kiasi cha shilingi milioni 172.5 ambazo vilikopeshwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu katika mwaka wa 2019/20.

Alisema kwa vikundi ambavyo vitashindwa kurejesha fedha hizo wachukuliwe hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani ili pesa zirudishwe kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine.

 

ACP Advera alisema sanajari na hilo ni lazima Menejimenti ihakikishe inafuatilia wadaiwa  wa mashine za kukusanyia Mapato (POS) ili waweze kurejesha kiasi cha 109.7 na kuwachukulia nyingine.

 

Katika hatua nyingine Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya kuhakikisha kila wanapokusanya fedha za mapato yake ya ndani kuhakikisha kuwa wanatenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na asilimia 10 kwa ajili ya kuvikopeshwa vikundi.

 

Alisema hatua itawasaidia kuepuka hoja za kikagua ambapo katika mwaka 2019/20  kiasi cha shilingi 332.3 kilikusanywa lakini hakikupelekwa       kwenye miradi ya maendeleo.