Home Mchanganyiko MIGOGORO IKIKOSA SULUHU HUONDOA AMANI ,TUPAMBANE KUTATUA MIGOGORO-FATMA

MIGOGORO IKIKOSA SULUHU HUONDOA AMANI ,TUPAMBANE KUTATUA MIGOGORO-FATMA

0
**************************
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji

MRATIBU wa miradi ,kutoka shirika la Search for Common Ground ,Fatma Kimaro ,ameeleza ,endapo migogoro midogo, ikiwemo ya ardhi ,wakulima na wafugaji pamoja na ndoa haipati suluhu  kikamilifu basi hugeuka kuwa mikubwa na kufikia hatua ya kuvunja amani.

Kutokana na hilo ,ameiasa jamii kuheshimiana na kufuata sheria za nchi ikiwa ni sambamba na mamlaka husika kusimamia sheria na kutenda haki ili kupunguza migogoro hiyo.

Fatma alisema, shirika hilo kwa kushirikiana na washirika wake HLRC na ZLC wanaendesha mradi wa JENGA AMANI YETU ,ambao umefadhiliwa na European Union,mradi ambao unalenga kutoa elimu ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani.

Alieleza hayo ,wakati walipozikutanisha asasi za kiraia na waandishi wa habari wanaofanya shughuli zao maeneo ya Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Fatma alifafanua ,mafunzo haya ya jinsi ya kushughulikia migogoro ya kijamii, Hii ni kwa sababu mara nyingi migogoro midogo midogo isiposhughulikiwa kikamilifu na dalili zake hugeuka machafuko na kuhatarisha amani kupotea .

“Ili kutafuta suluhu la kudumu la migogoro ya mara kwa mara, shirika hili limewajengea uwezo makundi hayo,  juu ya namna za utatuzi wa migogoro kisheria.”

“Kutafuta suluhu ya muda mrefu kupitia miradi kama huu,na hii ni kwa kuwa shirika hili linaamini amani ni msingi wa maendeleo wa nchi yoyote ile.” Aliongeza fatma.

Mratibu huyo ,alisema kupitia ushirikiano na ,ushawishi wa waandishi wa habari na asasi hizo wanaweza kusaidia kuleta matokeo chanya na kupunguza migogoro hii.

Hata hivyo Fatma alibainisha, mradi huo wa Jenga Amani Yetu unatekelezwa Pwani, Tandahimba,Mtwara,Tarime,Zanzibar na Pemba ambapo pia ipo miradi mingine mitatu ukiacha huu unaojikita na vijana ,ulinzi na usalama,asasi za kiraia na ule unaotoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Nae mshiriki wa mafunzo hayo ,kutoka asasi inayoshughulika na kutoa msaada wa kisheria ,la Jicho angavu foundation huko Kibiti ,Hussein Mikulu alisema, Jukumu lao lingine ni kusambaza elimu ya umuhimu wa amani na usalama kwenye maeneo yetu.  

Alibainisha ili kuleta maendeleo na amani kwa upande wa wafugaji na wakulima hawana budi kufuata sheria ya mpango wa matumizi bora ya ardhi na wafugaji wajue sio vyema kuachia mifugo ikala mazao ya wakulima na pia si vizuri baadhi ya wakulima kuuwa mifugo ya wafugaji.