Home Mchanganyiko RAIS SAMIA:”KUKAMILIKA KWA UJENZI WA RELI YA KISASA KUTALINDA BARABARA ZETU”

RAIS SAMIA:”KUKAMILIKA KWA UJENZI WA RELI YA KISASA KUTALINDA BARABARA ZETU”

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Karatasi yenye majina ya viongozi mbalimbali walioshiriki kufanikisha kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341 mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

……………………………………………………………………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutasaidia kulinda barabara zetu.

Kauli hiyo ameisema leo Juni 14,2021 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wakati jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341.

Rais Samia amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Reli ya kisasa itasaidia kulinda barabara zetu kama mnavyofahamu mizingo yetu inasafirishwa kwa magari hivyo kusababisha barabara nyingi kuharibika.

”Hasa baadhi ya madereva wamekuwa hawazingatie viwango vya uzito lakini tumeambiwa kuwa Reli nayo itakuwa na uwezo wa kusafrisha tani nyingi na ukiangalia tani zilizotaja ni 15 hadi 25 kwa wakati mmoja hiyo sawa na malori zaidi ya mia tatu”amesema Rais Samia

Hata hivyo amesema kuwa tutakuwa na barabara zenye ubora wa kudumu kwa muda mrefu pia reli hii itachangia kuchochea kitenga uchumi na uzalishaji hususani Kilimo Ufugaji,Uvuvi,Viwanda biashara bila kusahau utalii,kuna watalii watapanda Reli.

Vile vile amesema kuwa ndani ya reli kutakuwa na mabehewa maalum  yatakuwa yanabeba samaki na nyama na hivyo kuwanufaisha wakulima na wafugaji.

Rais samia amebainisha kuwa ujenzi wa reli hiyo utasaidia kupunguza gharama na usumbufu kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi na kulazimika kusafiri hadi mkoani Dar es Salaam kupokea mizigo yao.

Pia ameeleza kuwa wataendelea kutekeleza miradi ya kimkakati iliyoachwa na mtangulizi wetu Hayati Rais Magufuli ndio maana leo nipo hapa nafarijika  kuweka jiwe la msingi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza kwenda Isaka utazalisha ajira zaidi ya 86,000 kwa Watanzania.

 Kadogosa amesema ajira 11,000 zitakuwa za kudumu na ajira zisizo za kudumu zitakuwa zaidi ya 75,000.

Kwa mujibu wa Kadogosa, reli hiyo inayotoka Mwanza hadi Isaka  itakuwa na urefu wa kilometa 341, “ujenzi huu utagharimu Sh3.1 trilioni na tayari tumeshajenga kambi kwa ajili ya kuanza ujenzi huu.”

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei, Michael Zhang amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo inashirikiana na TRC kutoa vifaa vya mawasiliano na huduma kwenye mradi wa SGR ikiwemo Mfumo Teknolojia ya Mawasiliano-Reli (GSM-R), ambayo baadae itabadilika kuwa mfumo wa LTE- R.

“Niimani yetu kwamba chini ya uongozi mpya wa Rais Mama Samia Suluhu , Huawei itaendelea kujenga Miundombinu ya TEHAMA kulingana na Dira ya maendeleo ya Tanzania 2025,” ameahidi.